Home Kimataifa #2DaysToKiev, wakati Real Madrid wakimuwaza zaidi Mo Salah kuna huyu  James Milner

#2DaysToKiev, wakati Real Madrid wakimuwaza zaidi Mo Salah kuna huyu  James Milner

9115
0
SHARE

Bado tuko kwenye siku za mwisho kuelekea Champions League, bado siku mbili tu kufikia ile siku ya Jumamosi ambapo Real Madrid na Liverpool zitapepetana, Mo Salah na Cristiano Ronaldo watakuwa wakitizamwa sana katika mchezo huu.

Salah kwa sasa anatajwa kuingia katika orodha ya wachezaji watatu bora wa dunia, na uwepo wa Ronaldo kwa upande mwingine unawafanya watu kuamini hawa wataubeba mchezo huu, lakini huyu hapa ni James Milner.

Cristiano Ronaldo anakwenda Kiev kama mchezaji mwenye umri mkubwa na huku Liverpool ni Milner, lakini kuna tofauti kubwa ya meters walizocover uwanjani wawili hawa katika msimu wa Champions League na rekodi zinaoneaha Milner amekimbia meter 3590 zaidi ya CR7.

Katika mechi mbili tu vs As Roma, James Milner alikimbia uwanjani na kucover 26.57km kama ramani hapo chini inavyoonesha “alivyokichafua”, 

na mechi ya pili alifanyiwa vipimo vya kutumia madawa ya kuongeza nguvu michezoni na wengi wakidai ni kutokana na 13.57km alizokimbia katika mchezo wa pili kati ya As Roma vs Liverpool.

Hapewi heshima inayompasa kupewa lakini Milner amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Liverpool katika Champions League kuliko Epl, mechi dhidi ya As Roma aliivunja rekodi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na nyota wa Brazil Neymar.

Neymar ndiye alikuwa mchezaji mwenye assist nyingi zaidi katika Champions League lakini Milner aliifijia rekodi hiyo katika mechi dhidi ya As Roma ambapo sasa James Milner naye anakuwa na assists 8.

REKODI YA ASSIST NYINGI CHAMPIONS LEAGUE.

James Milner 8 2017/2018

Neymar 8  2016/2017

Ryan Giggs 7 2006/2007

Xavi 7 2008/2009

Mesut Ozil 7 2010/2011

Zlatan Ibrahimovich 7 2012/2013

Roberto Firminho 7 2017/2018

Madhara makubwa ya James Milner yanaonekana kuwepo katika michuano ya Champions League kuliko michuano ya EPL, katik EPL Milner amekuwa akitengeneza assist moja kwa kila baada ya dakika 588, wakati katika Champions League assist moja ni kila baada ya dakika 99.

Luka Modric, Toni Kroos, Isco, Marco Asensio na Casemiro wanatajwa na kuonekana viungo bora watakaoamua fainali hii kwa Real Madrid, lakini pamoja na uwingi wao kwa pamoja wamezidiwa assists 3 na James Milner.

Anaweza asiwe muhimu kwa Liverpool katika EPL kwani EPL anashika nafasi ya 8 kwa Liverpool katika assists lakini CL anashika ya 1, EPL pia anashika nafasi ya 8 kwa tackling lakini CL anashika ya 1, EPL anashika nafasi ya 5 kwa pasi kwa Liverpool lakini Champions League ya 3.

Zinedine Zidane na jopo lake la ufundi ni hakika wanajua rekodi za Milner na wameona fomu yake katika Champions League, na sasa Zidane anapaswa kutafuta namna ya kumzima Milner hapo keshokutwa, wakimuacha kama alivyoachwa na Roma inaweza kuwa shangwe Anfield.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here