Home World Cup Tiketi ya Bombadia: Messi kucheza kiwanja cha pili kwa ubora

Tiketi ya Bombadia: Messi kucheza kiwanja cha pili kwa ubora

7446
0
SHARE

Safari Ya Urusi….

Na: DANIEL S.FUTE

Inaendelea…. TUKIWA tunaelekea mwisho wa makala hii, kuhusu viwanja 12 ambavyo vitatumiwa katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018. Ni kuambie kwamba tayari timu zote 32 ambazo zitashiriki fainali hizi wamekamilisha kutaja majina ya vikosi vyao ambavyo vitaenda kupambana Urusi.

Kinachosubiriwa sasa ni siku tu ya kuanza kwa fainali hizi. Tusonge mbele na muendelezo wa makala hii, ambapo inatarajia kumalizika siku ya kesho.

Leo tutakizungumzia kiwanja cha kumi na moja, baada ya Volgograd tulicho kizungumzia siku ya jana.

*Spartak (Otkritie Arena)*

Otkritie ni Uwanja mpya uliofunguliwa hivi karibuni katika mji wa Moscow. Uwanja huu ambao unamilikiwa na klabu ya Spartak Moscow katika mechi zake za nyumbani, utatumika pia katika mechi za fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Awali klabu ya Spartak katika historia yao ya nyuma walikuwa hawana umiliki wa uwanja mzuri, hivyo walikuwa wanatumia viwanja mbalimbali katika mji wa Moscow pamoja na uwanja wa Luzhniki.

Klabu hiyo ilikuwa na mpango wa kujenga Uwanja wao mpya tangu mwaka1990, lakini mipango yao haikufaulu. Hadi kufikia mwaka 2005 ambapo mradi rasmi wa kujenga Uwanja huo ulipo patikana na kupata nafasi ya kujenga Uwanja huo katika Uwanja wa ndege wa Tushino huko kaskazini-magharibi mwa Moscow.

Mafanikio machache yalifanywa katika ujenzi huo, lakini kufikia mwaka 2008 mgogoro wa kifedha ulipelekea kupunguza kiasi cha gharama za ujenzi na ujenzi kusimama kwa muda.

Kufikia Julai 2010 ujenzi wa Uwanja huo ukaanza tena na sasa mipango ya kifedha ilikuwa bora zaidi. Mipango ya awali Uwanja huo uliwekwa idadi ya kuingiza watu 35,000, lakini baada ya Uwanja huo kuchaguliwa katika fainali za Kombe la Dunia ukaongezwa hadi kufikia idadi ya kuingiza watu 42,000.

Wilaya ya Otkritie ilithibitisha kuwa Uwanja huo ni wa pili wa michezo kwa ubora baada ya Luzhniki, katika mji wa Moscow. Tarehe 5 Septemba 2014 Uwanja wa Otkritie Arena ulifunguliwa rasmi katika mchezo wa Spartak na Red Star.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi tano tu, katika fainali hizo zitakazoanza hivi karibuni:

★16 June 2018 16:00 – Argentina vs Iceland – Group D

★19 June 2018 15:00 – Poland vs Senegal – Group H

★23 June 2018 15:00 – Belgium vs Tunisia – Group B

★26 June 2018 17:00 – Serbia vs Brazil – Group C

★3 July 2018 21:00 – 1H vs 2G – Round of 16

Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika uwanja wa Otkritie Arena, Usikose kesho katika tamati ya makala hii ya viwanja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here