Home Kimataifa #RoadToRussia: Fahamu mataifa yalizoshiriki kombe la dunia na kucheza michezo mingi

#RoadToRussia: Fahamu mataifa yalizoshiriki kombe la dunia na kucheza michezo mingi

7633
0
SHARE

Brazil ndiyo taifa pekee ambalo limeshiriki fainali zote 20 za kombe la dunia na fainali za mwaka huu zitakuwa ni fainali za 21.

Katika mara 20 zilizopita, Brazil imecheza michezo 104 ikifuatiwa na Ujerumani ambayo imeshiriki mara 18 na kufanikiwa kucheza michezo 106.

Italy ambayo mwaka huu haijafuzu fainali za kombe la dunia imeshiriki mara 18 na kucheza michezo 83 huku Argentina ikiwa imeshiriki mara 16 kwenye fainali hizo na kucheza michezo 77.

Hispania imefanikiwa kushiriki mara 14 kaika fainali hizo na kucheza michezo 59 wakati England nayo ikiwa imeshiriki mara 14 na kufanikiwa kucheza michezo 62 kwenye michuano hiyo.

Ufaransa imeshiriki kombe la dunia mara 14 sawa na England pamoja na Hispania na imecheza michezo 59 na mabingwa wa kwanza ambao pia ni wenyeji wa kwanza wa michuano hiyo Uruguay nayo imeshiriki mara 12 na imecheza michezo 51.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here