Home Kitaifa Ndanda yafufua matumaini kubaki ligi kuu

Ndanda yafufua matumaini kubaki ligi kuu

8730
0
SHARE

Ndanda mepata ushindi wa pili kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona katika mechi za VPL msimu huu baada ya kuifunga Mwadui 3-0, kabla ya mchezo wa leo Ndanda ilikuwa imeshinda mchezo mmoja tu kati ya 13 iliyochezwa kwenye uwanja huo.

Ushindi huo umefufua matumaini ya Ndanda kubaki ligi kwa msimu ujao, imefikisha pointi 26 na kusogea juu kwa nafasi mmoja kutoka nafasi ya 15 hadi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Mechi za mwisho ndio zitaamua timu ipi kati ya Ndanda na Majimaji itakayoungana na Njombe Mji kuiaga ligi kuu Tanzania bara.

Ndanda itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona-Mtwara mechi ambayo itaamua hatma ya Ndanda kubaki ligi kuu au kushuka kwenda ligi daraja la kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here