Home Featured UKURASA WANGU Martial na Lacazette walistahili dhahabu sio mawe

Martial na Lacazette walistahili dhahabu sio mawe

14064
0
SHARE
Didier Deschamps ametaja kikosi chake.

Wana kikosi kizuri sana, bila shaka kikosi chao kinaweza hata kufika hata fainali za kombe la dunia. Kuna uwezekano kwamba kuna baadhi ya wachezaji wameitwa lakini aidha hawakustahili au walioachwa walikuwa bora zaidi ya hao walioitwa.

Nimeona Benjamini Mendy ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.

Nimewaza sana hasa ni ipi sababu kubwa ya kuitwa kwake? Je ni mchezaji tegemezi sana timu ya taifa?? Mhh.. sina uhakika sana maana amecheza michezo mitatu tu timu ya taifa. Mendy karibia msimu mzima yupo benchi kwa majeruhi.

Sasa ni nani alistahili? Lucas Digne au Jordan Amavi au Kurzawa

Jordan Amavi amekuwa na kiwango bora kwa Klabu yake ya Marseille ambao walifika hatua ya fainali ya kombe ligi ndogo barani ulaya maarufu kama Yuropa. hatuwezi kumuongelea sana maana hayupo kabla kubwa wala ligi bora.

Takwimu za Amavi
Mechi Magoli asisti dakika
42 1 7 3462

Mendy ametumia Zaidi muda mwingi kama majeruhi. Lucas Digne angalau amecheza dakika 702 lakini tunaweza kukiri kuwa Barceona palikuwa na ufinyu wa yeye kuanza.

Tukiachana na hao, Aymeric Laporte ameachwa kisha ameitwa bwana mdogo mwingine wa Stuttagatt Benjamini Pavard. Hichi nacho ni kioja. Labda Deschamp ameridhika na kiwango cha Umtiti pamoja na Varane hivyo anajiamini Zaidi. Benchi atasubiria mzee Rami pamoja na kijana huyu Pavard.

Wapo wanaodai kuwa Laporte mechi za mwisho za Man City amezingua. Nachodhani mimi kuzingua ni kawaida sana hasa kwa mchezaji aliyehamia timu mpya. Kama kigezo ni kufungwa na Liverpool watakuwa wanamuonea maana makosa mengi alifanya Company na Otamend.

Nimeangalia takwimu za Pavard, Rami na Laporte

Laporte (22) Pavard (22) Rami (32)
Michezo 38 34 50
Pasi 92% 83% 83
Magoli 1 1 2
Asisti 3 0 2
Mipira ya juu 4 3 2
Kubloku 0.7 1 0.6
kuokoa 4.9 5.4 4.8
kudribo 0.7 0.3 0.6
takolini 2 1.6 1.1
kuingilia 1.4 2.1 1.4
Takwimu jumla 7.7 7.10 6.98

Kwanini nawakataa Pavard na Rami, licha ya kwamba wamelingana kwa kiasi Fulani na Laporte? Laporte ana uzoefu mkubwa wa mechi kubwa na hivyo amepata uwezo wa kupambana katika mashindano makubwa. Pavard amecheza michezo 37 hakuna hata mmoja aliotoka nje ya Ujerumani. Amekuwa akiipigania klabu yake ndani ya Bundasliga pekee.

Laporte amecheza ligi mbili ndani ya msimu mmoja hivyo amecheza Zaidi ya makombe matano tofauti. Rami umri umeenda. Sikuona haja ya kumuuita na kupuuza ujio wa Laporte. Sawa Rami ni mzee ana miaka 32 labda tunahitaji busara za wazee lakini naamini uwepo wa Matuid kwenye timu ulitosha.

Rabiot nae katemwa. Ameitwa Matuidi. Sawa matuidi ni mzuri na ni mzoefu. Rabiot hata kama angeenda uwepo wa Pogba na Kante bado hautampa chumba cha kubadilishia nguo. Inawezekana kweli Matuidi kasi yake imepungua.

Hata mimi nakiri Matuidi ameitwa tu kwa busara.

Aina yake ya uchezaji ndiyo inayopunguza kasi yake uwanjani. Kwa rabiot sina neon wala sitaki kuingilia maamuzi ya Deschamps. Pole sana Rabiot.

Shida ipo hapa kwa Martial na Dembele.

Niseme tu nilionao moyoni mwangu. Dembele sio wa kucheza klabu kubwa kama Barcelona. Mimi uwezo wake namuona kama Zaha tu. Barcelona walipaniki sana kumnunua hasa baada ya kumpoteza Neymar.

Dembele hakustahili kiasi kile wala hastahili kucheza kikosi cha kwanza cha Barcelona. Nimeshangaa sana Deschamps kumchukua kwa kigezo kuwa Martial amefanya vibaya.

Nmejiuliza sana ubaya wa Martial ni upi bado siajapata jibu.

Takwimu

takwimu Dembele Martial
Mechi (dakika) 16 (1021) 28 (1927)
Magoli 4 12
asisti 6 7
pasi 82% 83%
kukimbia 1.2 1.6
Kutengeneza nafasi 20 30
mashuti 64 62

Sijaona sababu za msingi za kumtema Martial. Licha ya kwamba Martial alicheza michezo michache katika kikosi cha Man United, kwenye michezo ya ligi kuu alitokea benchi michezo 12 kati ya 18 na kufunga magoli 9. hakuna mchezaji mwingine Zaidi ya Lukaku aliyemzidi magoli hata katika kikosi cha Barcelona ukitoa Messi na Suarez hakuna aliyemfikia magoli Martial.

Kwanini dembele aliyekuwa majeruhi aanze?

Kuna mtu ameniambia Martial ni mjeuri. Kwa wale wanaofuatailia mpira wa miguu kwa siku nyingi utajua kuwa fika kwamba Martial yupo katika hali gani. Mourinho sio kocha kwenye uso wa soka la hela. Binafsi huwa napingana sana na njia anazotumia kuwakosoa wachezaji wake.

Mambo yanapokuwa magumu Mourinho huwa anatafuta mchezaji wa kumbambikizia lawama. Amekuwa akimtumia Martial kama Chambo. Lakini kwa mashabiki wa Man United hawawezi kudharau nafasi ya Martial hasa kwa kile alichofanya msimu wake wa kwanza.

Martial hajawahi kuwa jueri lakini hakuna mchezaji ambaye yupo tayari kupelekeshwa hasa katika dunia hii ya hela. Nadhani mnakumbuka msimu wa Mwisho wa Mourinho Chelsea. Namna alivyosumbuana na Hazard. Kiwango cha Martial ni kikubwa sana kuzidi cha huyu Dembele. Kilichopo tu ni namna mwalimu anavyotumia hisia zake kuchagua wachezaji badala ya kutumia uwezo.

Deschamp huyu huyu aliyesema Pogba hana furaha Man United hasa baada ya kuonekana kiwango kinashuka. Lakini ni Deschamp huyu huyu ambaye haoni kama Martial hana furaha Man United ila anaona kiwango chake ni kibovu kiasi cha kumchukua aliyetokea majeruhi

Kuhusu Giroud na Laccazete.

Wapo wanaoamini Giroud ni bora timu ya taifa. Huwa nachekaga sana nikisikia hizi hadithi. Giroud hajawahi kuwa mchezaji mzuri mbele ya macho yangu. Kufunga kwake ni kwa muhimu lakini sio mchezaji wa muhimu kwenye timu.

Giroud amefunga magoli 30 katika mechi 71 za Ufaransa sawa. Lakini magoli yake 20 amefunga kwenye mechi za kirafiki ambazo hazina tija wala haziwezi kupima uwezo wa mtu. Hizo mechi za kucheza na akina Cyprus huko sijui Luxembourg unataka kuniaminisha zinafanya Giroud awe bora mbele la Laccazette? namba hazidanganyi

Takwimu

Magoli Ndani ya Miaka
Giroud 69 5
Laccazete 73 3

Magoli mengi kwa msimu
Giroud 16
Laccazette 28

Kwa miaka mitatu Laccazette ameweza kutengeneza nafasi Zaidi ya 35 kwa msimu na kufunga Zaidi ya magoli 20 kwa msimu na mchezaji pekee aliyeweza kufanya hivyo ni Messi tu. Giroud ni aina ya washambuliaji wa zamaniiiiii sana. Washambulaiji wa nguvu na nafasi. Giroud sio mchezaji mzuri hata kidogo nje ya boksi.

Laca anakupa kila kitu.

Dunia ya sasa inahitaji washambuliaji kama Laca. Msimu ya mwisho Laccazette alikuwa na wastani wa pasi 71% nje ya eneo la penati na alikamilisha pasi 1517, Giroud alikuwa na pasi 619 tu na mbaya Zaidi ana asilimia 60 ya pasi nje ya eneo la hatari. Giroud hakuwahi kuwa bora mbele ya Lacca labda kuanzia 1991 kurudi nyuma kabla sijazaliwa.

Kuna watu wanasema Laccazete ana takwimu mbaya msimu huu ukilinganisha na Giroud. Namba hazidanganyi.
Dakika Magoli Goli kwa dkk asisti
Giroud  2157  12 179.8 1
Laccazette  2758  17 149.5 4

Sioni sababu za kuamini kuwa Lacazette eti hana madhara makubwa kama aliyo nayo Giroud. Binafsi yangu ukiweka Giroud na jiwe sokoni nitanunua jiwe. ni mmoja wa washambulaiji wazembe na wabovu. Wanafunga kwa sababu tu wanacheza eneo la kufunga. Smalling na Giroud hawana tofauti kiuchezaji ila wanatofautiana tu maeneo wanayocheza.

Makala hii imeandaliwa na Privadinho unaweza kunifollow Instagram kwa jina hilohilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here