Home Dauda TV Video-Yanga imemaliza ukame wa dakika 810 bila ushindi

Video-Yanga imemaliza ukame wa dakika 810 bila ushindi

7136
0
SHARE

Yanga imehitimisha dakika 810 bila ushindi katika mashindano yote baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbao kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa taifa.

Goli pekee la kiungo wa kimataifa Thaban Kamusoko dakia ya 26 limeipa Yanga ushindi ambao ulisubiriwa kwa muda mrefu.

Yanga ilicheza mechi tisa (dakika 810) bila kupata ushindi, imetoka kupiteza mechi nne mfululizo kabla ya sare mbili (VPL), imepoteza michezo miwili ya kimataifa na sare moja (CCC).

Mechi tisa (dakika 810) za Yanga bila ushindi

  • Yanga 1-1 Singida United
  • Welayta Dicha 1-0 Yanga
  • Mbeya City 1-1 Yanga
  • Simba 1-0 Yanga
  • USM Alger 4-0 Yanga
  • Tanzania Prisons 2-0 Yanga
  • Mtibwa Sugar 1-0 Yanga
  • Yanga 0-0 Rayon Sports
  • Mwadui 1-0 Yanga

Baada ya mchezo huo Yanga imefikisha pointi 51 ikiendelea kubaki katika nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 28 ikibakiza mchezo mmoja mkononi (kiporo).

Kwa mujibu wa ratiba, mechi ijayo Yanga itacheza dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here