Home World Cup Tiketi ya bombadia: Mo Salah ataanzia kiwanja hiki

Tiketi ya bombadia: Mo Salah ataanzia kiwanja hiki

7507
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

Inaendelea…. FAINALI za Kombe la Dunia ni fainali zenye msisimko mkubwa sana kila zinapofika wakati wake. Lakini pia ni fainali zenye kuleta mshangao kutoka kwa wachezaji, makocha hadi mashabiki.

Zimebakia siku chache kuanza kwa fainali hizi lakini tayari imejitokeza mishangao mbali mbali ambayo watu hawa kuitarajia, labda wailitarajia kuiona pindi mashindano haya yatakapoanza Juni 14.

Acha tusonge na muendelezo wa makala yetu kuhusu viwanja maalumu kwaajili ya fainali hizi. Na leo tunaenda katika kiwanja cha kumi na kubakiza viwanja viwili.

*Volgograd*

Volgograd ni Uwanja ambao umejengwa ndani ya mji wa Volgograd, katika nchi ya Urusi kwaajili ya mechi za fainali za Kombe la Dunia.

Uwanja huu upo eneo la Kusini mwa taifa la Urusi. Na lengo kubwa kujengwa kwa uwanja huu ni kwaajili ya Kombe la Dunia pamoja na matumizi ya klabu ya mji huo wa Volgograd.

Volgograd ni uwanja mpya kabisa, hapo awali kulikuwa na uwanja katika mji huo lakini ulionekana si sahihi kwa kufanyika kwa mechi za Kombe la Dunia. Hivyo mwishoni mwa mwaka 2014 Halmashauri ya mji huo waliamuru Uwanja huo ubomolewe na ujengwe mpya.

Kufikia mwanzoni mwa mwaka 2015 ujenzi mpya wa Uwanja wa Volgograd ulianza kujengwa, na ramani yake ikawa inaeleza kwamba itaweza kuingiza idadi ya watu 45,000. Ambapo hii ni tofauti na ule ambao waliubomoa.

Kufikia mwaka 2017 Uwanja huu ulikamilika kwa asilimia zote. Mamlaka ya umiliki katika kiwanja hiki walisema kwamba, baada ya fainali hizi uwanja wa Volgograd utapunguzwa idadi hadi kufikia kuingiza watu 35,000.

Volgograd upo karibu na mabonde ya mto Volga, mto ambao unapita katikati ya mji wa Volgograd. Uwanja pia utakuwa uwanja mpya wa klabu ya Fc Rotor Volgograd inayokipiga katika Ligi kuu.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi nne tu, katika fainali hizo zitakazoanza wiki mbili zijazo:

★18 June 2018 21:00 – Tunisia vs England – Group G

★22 June 2018 18:00 – Nigeria vs Iceland – Group D

★25 June 2018 17:00 – Saudi Arabia vs Egypt – Group A

★28 June 2018 17:00 – Japan vs Poland – Group H

Hizi ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika uwanja wa Volgograd, Usikose tena siku ya kesho na muendelezo wa makala hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here