Home Kitaifa Manara kaeleza kilichompata baada ya Okwi kukosa penati

Manara kaeleza kilichompata baada ya Okwi kukosa penati

8732
0
SHARE

Juzi kati Simba ilicheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo ambao ulikuwa na sherehe na shamrashamra za mabingwa wapya wa ligi kuu   Simba kukabidhiwa kombe lao na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Siku iliyofuata kwenye mitandao ya kijamii kulizagaa video ikimuonesha Haji Manara akiugulia maumivu baada ya penati ya Emanuel Okwi kuokolewa na Juma Kaseja katika dakika ya mwisho.

Kumekuwa na maswali mengi juu ya tukio hilo kwamba nini kilimkuta Manara huku wengine wakihofia huenda ilikuwa ni issue ya kiafya ili Manara apewe ushauri.

Manara mwenyewe amefunguka na mwanzo mwisho nini kilimpata hadi kuugulia maumivu.

“Penati zikiwa zinapigwa kwa dakika zile huwa siangalii, iwe tunapigiwa au tunapiga huo ndio utamaduni wangu, baadaye huwa naangalia marudio nikiwa nyumbani.”

“Ilitokea penati dakika ya 90 sikuangalia niligeukia pembeni, sasa bahati mbaya au nzuri kwa pembeni alikuwa amekaa Mhidin Michuzi ambaue ni mpiga picha wa Ikulu kumbe alikuwa anarekodi tukio lote la mimi kutoangalia penati na baada ya Kaseja kupangua penati.”

“Uzuri Michuzi ni muungwana akaniuliza kama nipo tayari airushe na mimi nikaruhusu aiachie kuwahabarisha wananchi. Nimeona ime-trend sana kiasi ambacho sikutegemea lakini ni mambo ambayo huwa yananikuta.”

“Kwenye mpira inapokuja mechi kubwa kama ile  kwa sababu tulikuwa tunakabidhiwa kombe tulishacheza bila kupoteza kwa hiyo kupoteza mechi ile nilipata mshtuko kwa bahati nzuri niliweza kuumudu palepale mwenyewe.”

“Isiwape tabu wapenzi nipo vizuri kabisa ilikuwa ni jambo la dakika tano au sita tu. Unajua wengine tuna mapenzi ya kupitiliza ukiachana na kazi yangu mimi nina mapenzi makubwa sana na Simba. Nafanya kazi kwenye klabu ninayoipenda, nafanya kazi ninayoipenda.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here