Home Kitaifa IMETHIBITISHWA: Pluijm anaondoka Singida United

IMETHIBITISHWA: Pluijm anaondoka Singida United

8773
0
SHARE

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amethibitisha kwamba baada ya msimu kumalizika kocha wao mkuu Hans van Pluijm ataachana na club hiyo.

“Ni kweli kwamba kocha wetu Hans van Pluijm ataondoka kwenye klabu yetu kwa sababu ameomba kuondoka na tumefikia makubaliano. Tunampenda kocha wetu lakini hatuna namna kwa sababu ni makubaliano kati ya pande mbili”-Festo Sanga.

“Ni faraja kwetu kufanya nae kazi, Singida United inayozungumzwa leo ni kwa sababu ya kocba Hans, uwepo wake ndani ya klabu umeifanya iwe na jina kubwa tunajivunia na tunafurahia kufanya nae kazi na tunaamini ipo siku atarejea.”

“Kwa sasa tu ajiandaa na tuna CV za watu wengi sana wanaoomba nafasi ya kufanya kazi na Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu lakini makocha wakubwa wanaigombania kuja kufundisha.”

Azam imekuwa ikihusishwa kumalizana na Pluijm na taarifa zinasema kwamba atajiunga na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao kuchukua nafasi ya mromania Aristica Cioaba.

Pluijm ameisaidia Singida United kuwa nafasi ya tano kwenye VPL hadi sasa ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 29 wakati huohuo timu ikiwa hatua ya fainali ya kombe la TFF (Azam Sports Federation Cup) ambapo itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar Juni 2, 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here