Home Kimataifa Tukimtumia vizuri Samatta tutavuna mkwanja

Tukimtumia vizuri Samatta tutavuna mkwanja

9623
0
SHARE

Sports ni eneo ambalo hata wenzetu wanalitumia kutangaza vivutio vya utalii wa maeneo husika kwa sababu sports inakwenda mbali zaidi. Wanamichezo wanakwenda kushiriki mashindano tofautitofauti kama Olympics, Madola, kombe la dunia.

Wapo wanamichezo wengine ambao wapo nje, kwa mfano unaweza kumtumia kwa ajili ya kutangaza utalii na vivutio vya ndani kwa sababu kuna watu wengi wanaomfuatilia kule.

Kuna mzungu mmoja alikuja Zanzibar lakini Samatta ndio ilikuwa sababu ya yeye kuja, alitoka Genk Ubelgiji. Baada ya kumfatilia Samatta na kujua anatoka Tanzania halafu Zanzibar inavivutio vya kitalii akaamua kuja kutembea likizo yeye na familia yake.

Sasa ukiwekeza kwa mtu kama Samatta na ukawa na mpango mkakati wa kumtumia pamoja na fursa nyingine za michezo.

Nimesikia bondia muingereza Anthony Joshua anataka kuja Tanzania Ngorongro, Serengeti na Zanzibar wakajaribu kupitia kwenye mamlaka husika lakini kuna mahali walikwama. Kampuni ambayo inamwakilisha wakapata mawasiliano yangu wakanitafuta lakini nilichofanya nikawaahidi kuwapeleka kwa wahusika kwa sababu jambo hili siwezi kulibeba mwenyewe.

Kwa hiyo nikawatambulisha Ngorongoro na watu wa Wizara husika, nikawa nawaza kuhusu sports tourism na namna ambavyo Anthony Joshua alivyotayari kutumika na mamlaka kwa ajili ya kutangaza utalii wetu na impact yake itakavyokuwa kubwa kwetu.

Kuna wanamichezo huwa wanakuja lakini kwa siri kubwa kwa mfano David Beckham lakini Joshua yupo tayari kujitangaza kwamba nakwenda Tanzania na vyombo husika vimtumie.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here