Home World Cup Tiketi ya bombadia: Ronaldo atacheza hapa?

Tiketi ya bombadia: Ronaldo atacheza hapa?

7780
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

Inaendelea…. HADI sasa zimesalia wiki mbili tu kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia. Vile vile nitakuwa nimebakiza viwanja vitatu ambavyo vitatumiwa katika fainali hizo, kwaajili ya kuvizungumzia katika makala hii.

Leo tunasonga tena na muendelezo wa kiwanja cha tisa, baada ya Samara Arena.

Mordovio Arena

Mordovio Arena ni Uwanja ambao umegawanyika katika majina matatu tofauti tofauti. Wapo wanaopenda kuita Stadion Yubileyny, wengine wanautaja Uwanja wa Saransk.

Lakini katika fainali hizi za Kombe la Dunia, Uwanja huu utajulikana maarufu kwa jina la Saransk. Saransk ni mji mdogo sana ambao upo katika mkoa wa Mordovia, ndio maana wapo watu wanauita uwanja huu kwa jina la Saransk.

Uwanja huu umejengwa katika ya mji ambapo inapelekea mashabiki na watu mbalimbali kufika katika uwanja huu kwa hali yoyote ile. Wapo wanaoweza kufika kwa kutumia baiskeli, miguu, treni na magari.

Saransk ulianza kujengwa mwishoni mwa mwaka 2011. Hata hivyo kazi ya kujenga Uwanja huo uliendelea polepole sana, kulingana na miundombinu na ukosefu wa fedha. Hivyo ujenzi huo ukalazimika kusimama.

Mwishoni mwa mwaka 2014, ujenzi huo ulianza rasmi tena ambapo safari hii hawakusita tena hadi walipo ukamilisha mwaka 2017. Uwanja huu utakuwa na uwezo wa kuingiza idadi ya watu 45,000 kwa kiwango cha FIFA, lakini baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia uwanja utashushwa hadi kufikia viti 28,000.

Baada ya fainali za Kombe la Dunia, Uwanja huu utatumiwa na klabu ya Fc Mordovia Saransk kwa mechi za nyumbani na utakuwa unaitwa Uwanja wa Mordovia Saransk.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi nne tu katika fainali hizo zitakazoanza wiki mbili zijazo:

★16 June 2018 19:00 – Peru vs Denmark – Group C

★19 June 2018 18:00 – Colombia vs Japan – Group H

★25 June 2018 21:00 – Iran vs Portugal – Group B

★28 June 2018 21:00 – Panama vs Tunisia – Group G

Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika Uwanja wa Saransk, Usikose tena siku ya kesho na muendelezo wa makala hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here