Home Kimataifa #RoadToRussia, unapaswa kuyajua haya muhimu kuhusu Hispania

#RoadToRussia, unapaswa kuyajua haya muhimu kuhusu Hispania

8070
0
SHARE

Wahispania nao wametangaza jeshi lao linalokwenda kupambana nchi Urusi mapema mwezi ujao katika kombe la dunia, wachezaji wengi mastaa wamemwagwa lakini kutoka EPL ni nyota wanne tu ndio wanakwenda Urusi.

Nani mzoefu zaidi katika kikosi? Sergio Ramos pamoja na kwamba umri haujakwenda sana lakini ndio mzoefu katika kikosi cha Hispania akiwa amecheza mechi 151 lakini Kepa Arrizabalaga ameitwa katika kikosi hiki akiwa amewahi kuichezea Hispania mechi 1 tu.

Mji uliotoa wachezaji wengi zaidi. Madrid ndio mji ambao umetoa wachezaji wengi zaidi David De Gea, Pepe Reina, Dani Carvajal, Nacho and Koke(5), huku Barcelona ikiwatoa Jordi Alba, Gerard Pique and Sergio Busquets, laki wapo pia wachezaji ambao sio wazawa wa Hispania Thiago ni mzaliwa wa Bari nchini Italy, Diego Costa na Rodrigo Moreno wamezaliwa Brazil.

Nani babu na nani mtoto. Kila mtu aliposikia Pep Reina ameitwa walijua ameitwa kwa sababu ya uzoefu, na ni kweli Reina ndio mchezaji mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 38 huku kinda wa Real Madrid Marco Asensio anakwenda Urusi akiwa na miaka 22.

Nani kinara wa mabao? Ni David Silva, kiungo huyu wa Manchester City anakwenda Urusi kama kinara wa mabao katika timu ya Hispania. Silva hadi hivi sasa ana mabao 35 akifuatiwa na Iniesta ambaye ameshaweka kambani mabao 14.

Kama ulikuwa hufahamu tu ni kwamba wachezaji 17 kati ya 23 wa kikosi cha Hispania wanacheza ligi ya nchini kwao Hispania, ni David De Gea, Cesar Azpilicueta, David Silva, Nacho Monreal(EPL), Pep Reina(Serie A) na Thiago Alcantara(Bundesliga).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here