Home Kimataifa Mrithi wa Arsene Wenger huyu hapa na makombe yake

Mrithi wa Arsene Wenger huyu hapa na makombe yake

10401
0
SHARE

Zilianza kama tetesi kwamba kocha aliyepita wa PSG Unai Emery atachukua mikoba ya Arsene Wenger pale Arsenal, lakini moja kati ya vikwazo vikubwa kwa Emery ikawa ni lugha na inadaiwa Emery hafahamu Kingereza.

Arsenal wakawa mbioni kumtangaza Arteta kama mrithi wa Wenger lakini sasa habari zimebadilika, katika masaa machache au siku chache zijazo Emery anaweza kutangazwa kama kocha mpya Gunners.

Wengi wameanza kudai kwamba Emery sio kocha sahihi kwa Arsenal lakini ukweli ni kwamba Emery ni kocha ambaye yuko tofauti saba na Wenger kwani ni kocha ambaye hana uhaba wa makombe.

Achilia mbali ametoka kuwapa ubingwa wa Ligue One klabu ya PSG lakini Emery ni amewahi kuchukua kombe la Europa League back to bach mara tatu akiwa na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania.

Ukiacha Ligue One, Emery pia amewahi kushinda makombe manne akiwa na PSG. Ameshinda kombe la French Ligue Cup mara 2 na PSG lakini pia ameshashinda kikombe cha French Cup mara mbili akiwa na PSG.

Katika msimu wa ligi wa mwaka 2013-2014 kocha huyu wa zamani wa PSG alishinda tuzo ya kocha bora wa vilabu barani Ulaya. Sasa kinachosubiriwa ni taarifa tu kutoka klabuni hapo Emery aanze kazi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here