Home Featured UKURASA WANGU Martinez Kumuacha Nainggolan ni funzo pevu kwetu

Martinez Kumuacha Nainggolan ni funzo pevu kwetu

8660
0
SHARE
Martinez amemtupilia mbali Radja Nainggolan kwenye kikosi cha Belgium.
kuna mwenye swali? una dukuduku?
Hii sio kwa mara ya kwanza RADJA NAINGGOLAN kuachwa kwenye kikosi hiki. Mchezaji huyu wa As Roma ameachwa na Roberto Martinez kwenye kikosi cha wachezaji 28. Martinez amedai kuwa ameachwa kwa sababu za kiufundi.
Martinez “haya ni maamuzi ya kiufundi siwezi kumpa nafasi anayotaka kucheza uwanjani”
Mchambuzi wa Ubelgiji Kristof Terreur anakubaliana na mawazo ya Martinez lakini pia anaungana mkono na mimi. ukiachana na suala la ubora wa Nainggollan. kwenye soka kuna kitu kinaitwa NIDHAMU. Soka bila nidhamu haliendi. Mnamkubuka vizuri Baloteli?
Kuna tatizo lipo Argentine. Nafasi ya Dybala na Messi. Yupi acheze kama Advanced Playmaker (viungo wabunifu wa kisasa)?
Mchambuzi huyu anasema hivi
“Roberto Martínez amekuwa akimtumia Radja Nainggolan kama namba 10, kuliko kiungo wa dimba la juu au box-to-box nadhani hapo nimeeleweka.
Ikumbukwe kwamba…
Radja Nainggolan aliachwa na Roberto Martinez kwenye michuano ya awali ya kufuzu Kombe la Dunia. Katika nafasi ambayo Radja amekuwa akitumika ni ngumu sana kwake kufanya vizuri hasa katika mfumo huu wa mwalimu. Tatizo hili hata Lionel Messi amewahi kukiri kuwa hana shida na Dybala ila tatizo lipo kwamba mafanikio makubwa ya Dybala ameyapata kwa kucheza kiungo mbunifu wa kisasa ambao hutokea pembeni na kuingia kati na Mpira.
Dybala anatokea kulia sawa sawa na anavyocheza Messi.
Ni ngumu kwa mwalimu kumbadilisha mchezaji mfumo hasa hasa kwa timu ya taifa ambayo hawana muda wa kukaa kambini hivyo inakuwa kama ni riski.
Tatizo hili lipo kwa Ubelgiji ambapo namba 10 hutokea pembeni.
Mfumo wao ni 3-4-3 ambapo kama De Bruyne hatocheza nafasi ya namba 10 lazima ubutu katika safu ya ushambuliaji uonekane.
Je Radja atafiti wapi?
Je kwa Mfumo huu Radja atacheza wapi? Jibu ni rahisi sana,
Atacheza kwenye safu ya viungo pacha wa kati akisaidiana na Dembele.
Je kwanini mwalimu hajamuita na kwanini mwalimu alimlazimisha kucheza nafasi ambayo sio sehemu aliyozoea?
Jibu ni moja tu, Martinez kuna somo alitaka kutoa.
Martinezi sio mlevi. Hapendi sigara kabisa. Nainggolani ukimzuia sigara mtagombana maisha yenu yote.
Nainggolan, ana miaka 30, na amecheza mechi 29 kwa Belgium. Katika umri huu alipaswa awe amecheza takribani mechi 80 hasa kwa ubora wake. Lakini kazidiwa Hadi na Giroud mechi nyingi. Kumbe kutokuitwa sio gundu la Martinez.
Mfa maji haachi kutapatapa. Mwezi wa nane mwaka jana alitishia sana kujiuzulu baada ya Martinez kumtema. Alimtema kwenye michuano ya kufuzu.
Nimekumbuka sana sakata la Haruna Moshi Bobban na Mzee Marccio Maximmo.
Hakuna kitu kinatunza ufanisi wa mchezaji Kama nidhamu. Hata uwe na kipaji vipi kama huna nidhamu we ni kapuku tu. Ukiheshimu waalimu na ukaheshimu taaluma yako hakuna atakayekusumbua. Yale yale ya Akina Karim Benzema na Nicholaus Anelka.
Baada ya kutemwa hapo Martinez bado alionesha upendo na ukomavu. Akamuita tena kwenye mechi za kirafiki kati ya Mexico na ule wa Japan mwezi wa Novemba lakini alipatwa na majeraha.
Baadae alianza kusuasua mazoezini. Mazoezi ya mwisho ya timu ya taifa Martinez alimpigia simu na kumweleza ahudhurie bila kukosa. Lakini inasemekana kuwa Radja alipata taarifa kuwa ametemwa kwenye kikosi hivyo akaamua kupiga teke bakula mboga na kususa kula ugali mkavu.
Siku ya mazoezi ya mwisho Radja hakufika kabisa na hakutoa taarifa. Vipi ungekuwa wewe mwalimu ungefanyaje?
Ametemwa na ametuonesha kuwa yeye ni mchezaji bora ambaye mwalimu ameshindwa kummudu. Ukiweka samaki mmoja mbovu kwenye ndoo ataharibu wengine wazima. Kuna watu watalalamikia kuwa alipaswa kuitwa hivyo hivyo licha ya nidhamu mbovu.
Ukweli ni kwamba mchezaji mmoja akibebwa sana licha ya kuwa na nidhamu mbovu atafanya wachezaji wengine waone kuwa mwalimu hana kauli na pia mwalimu anampendelea. Hapa Tanzania hao watu wapo Sana wala sishindwi kuwataja kama akina Jonasi Mkude na Kevin Yondani.
Timu ya taifa ya Ufaransa ilivurugwa na akina Anelka na Evra mwisho wa siku ikafanya vibaya. Ukiwa na mchezaji asiye na nidhamu ni sawa na kuwa na saa mbovu kwenye chumba cha mtihani. Simba, Yanga na Stars zinakumbatia wachezaji walevi na wahuni kwa kigezo kuwa wana vipaji.
Mchezaji akiwa na kipaji kizuri lakini akawa na nidhamu mbovu ni sawa na pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe.

Maamuzi ya Nainggolan nayo vipi?

Ameandika ukurasa wake wa Instagram: “nimepatwa na shinikizo ambalo sio dhamira yangu kutundika daruga kwa taifa langu… nimejitolea kwa moyo wangu wote timu ya taifa kuhakikisha kuwa linasonga mbele, nimegundua kwamba kujikubali mwenyewe kunawaboa wengine. Kuanzia leo natangaza kwamba nitakuwa mshabiki namba moja wa taifa langu”
Martinez akaongeza kwamba.
kwa miaka miwili tumekuwa na wachezaji waliocheza kwa utaratibu maalumu. Kila mchezaji alikuwa na jukumu lake timu ya taifa bila kuangalia kwenye klabu yake anachezaje. Sipo tayari kuharibu utaratibu huo kwa sababu ya mchezaji mmoja.
Kila mtu anajua kipaji cha Radja. Radja ana majukumu makubwa sana kwenye klabu yake na amekuwa mhimili wa mafanikio ya As Roma lakini kwetu sisi Ubelgiji hatuwezi kumpa jukumu hilo” Mwisho wa kunukuu

Belgium wametangaza wachezaji 28- na watapunguzwa wengine watano:
Toby Alderweireld (Tottenham), Michy Batshuayi (Chelsea), Christian Benteke (Crystal Palace), Dedryck Boyata (Celtic), Yannick Carrasco (Dalian Yifang), Koen Casteels (Wolfsburg), Nacer Chadli (West Brom), Laurent Ciman (Los Angeles FC), Thibaut Courtois (Chelsea), Kevin De Bruyne (Manchester City), Mousa Dembele (Tottenham), Leander Dendoncker (Anderlecht), Marouane Fellaini (Manchester United), Eden Hazard (Chelsea), Thorgan Hazard (Borussia Monchengladbach), Adnan Januzaj (Real Sociedad), Christian Kabasele (Watford), Vincent Kompany (Manchester City), Jordan Lukaku (Lazio), Romelu Lukaku (Manchester United), Dries Mertens (Napoli), Thomas Meunier (Paris St Germain), Simon Mignolet (Liverpool), Matz Sels (Anderlecht), Youri Tielemans (Monaco), Thomas Vermaelen (Barcelona), Jan Vertonghen (Tottenham), Axel Witsel (Tianjin Quanjian).

UPI MTAZAMO WANGU
Nainggola ni mlevi wa kupindukia na mbaya zaidi ni mvivu na mropokaji. Kwenye mchezo wa Estonia alichelewa kufika mazoezini. 2014 hata Kocha Wilmots alimtema kwenye kikosi. Hakwenda kombe la Dunia kule Brazil. Wilmots anasema kuwa Radja alikuwa haingii uwanjani hajavuta sigara. Alikuwa anakera wachezaji wenzake kwenye Vyumba. Bodi ya Ubelgiji ikamkodishia chumba cha kuvutia sigara. Wilmots hakupendezwa na suala lile kabisa. Baadae Martinez nae hakuweza kumvumilia.
Huyu Jamaa mwaka 2016 Martinez alipimgia simu na kumwambia kwenye mchezo wa Gibralta ajiandae vyema. Kwenye mazoezi akafika jioni amelewa sana. Martinez akamtema na Ubelgiji wakashinda mabao 9 kwa 0 licha ya kwamba Witsel alipewa kadi nyekundu.
Radja amekuwa na tabia za kiswahili. Siku Moja Martinez alimpigia tena simu na kumweleza kuwa hatomjumuisha kikosini hivyo ajiandae vyema na abadilike sana ili aupime mwenendo wake kisha ampatie nafasi kombe la Dunia mwaka huu. Radja alikata simu wala hakumjibu akaenda moja kwa moja kwa waandishi wa habari na kusema maamuzi yale ni ya kipuuzi. Yeye ana kiwango kuliko Tielemens na Witsel.
Ukiwa na mwanajeshi mbeambea ambaye hawezi kuzuia mdomo wale kambi yenu itavamiwa.
Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here