Home Kitaifa Geoff Lea baada ya kusikia Shaabani Idd kafunga hat-treak

Geoff Lea baada ya kusikia Shaabani Idd kafunga hat-treak

9144
0
SHARE

Geoff Lea baada ya kusikia Shaabani Idd kaweka hat-treak jana kwenye mechi ya Azam 4-1 Tanzania Prisons hakuificha furaha yake na haya ndio yalikuwa maoni yake kuhusu uwezo wa Shaabani Idd Chilunda.

Hat-treak ya Shaabani Idd ni taarifa ambayo imenifurahisha, ni mchezaji ambaye namtazama kwa jicho la mbali sana namuona ni mshambuliaji ambaye amekamilika.

Tupo katika kipindi ambacho washambuliaji ni adimu sana, tunazungumzia kipindi ambacho msimu wa ligi barani Afrika unaisha ukitafuta wachezaji ambao wamekuwa wafungaji bora kwenye ligi zao kwa magoli 20 kwenda mbele unaweza kukuta hawazidi watano wakati mwingine imeshawahi kutokea walikuwa watatu.

Kuna utafiti naufanya msimu huu, mara ya mwisho kufanya utafiti kwenye ligi za Afrika ni Emanuel Okwi pekee ndio mshambuliaji mwenye magoli 20.

Shaabani Idd ni mchezaji ambaye katika umri wake ukiangalia aina yake ya uchezaji namuona ni mchezaji ambaye atafika mbali sana kama atapata management sahihi.

Imani yangu kwa wachezaji kama¬† Shaabani Idd ‘hawavundi’ kwenye ligi yetu kwa sababu tuna ushahidi mwingi wakati mwingine ligi yetu sio mahali pa mchezaji kucheza muda mrefu.

Naona kama Msuva alichelewa kuondoka labda angeondoka mapema zaidi lakini sio tatizo, Shaababi Iddi namuona anauwezo mkubwa sana kwa ile nafasi anayocheza ukiangalia magoli anayofunga hadi style yake.

Kitu kimoja ninachomtofaitisha na wachezaji wengine ni jinsi anapokuwa kwenye eneo la hatari na maamuzo anayochukua.

Shaabani Idd amefunga magoli sita (6) katika mechi nne za mwisho alizocheza. Aliathiriwa na majeraha ya muda mrefu mwanzoni mwa msimu, amerejea gari ndio limepamba moto ligi nayo ipo ukingoni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here