Home Kimataifa Chanya na Hasi kwa Liverpool kuelekea Kiev

Chanya na Hasi kwa Liverpool kuelekea Kiev

9609
0
SHARE

Zimebaki siku nne tu kwa Liverpool kujaribu kusimamisha utawala wa Real Madrid katika michuano ya Champions League, hii itakuwa ni fainali ya Champions League siku ya Jumamosi mjini Kiev.

Wengi wanaipa nafasi Real Madrid kutwaa tena taji hili kutokana na uzoefu wa wachezaji wao katika michuano hii, lakini Liverpool nao wanaonekana kuwa na kikosi ambacho kinatishia kila timu, yapo mambo Chanya na Hasi kwao kuelekea mchezo huu.

HASI.

Mbio ndefu pumzi kidogo. Pamoja na Liverpool kuonekana kuwa na strikers kiwembe lakini tatizo la ulinzi la Liverpool bado lipo haswa dakika za mwisho. Katika mabao 13 waliyofungwa katika CL msimu huu, mabao 6 yalifungwa katika dakika 20 za mwisho na kocha Jurgen Klopp amekiri tatizo la ulinzi. Wakati Liverpool wakiwa na tatizo kuruhusu mabao dakika za majeruhi, Real Madrid wanaonekana wazuri kuzimaliza timu pinzani dakika za mwisho(fainali 2014 vs Athletico Madrid).

Kiungo ya kati. James Milner na Jordan Henderson wako katikati katika kikosi cha Liverpool, na ni wazi kwamba hawa sio viungo bora kama aina ya viungo wanaoenda kukabiliana nao Kiev, Casemiro, Luka Modric na Toni Kroos ni world class midfilders na inaonekana wazi wanaweza wakaipoteza Liverpool uwanja mzima.

Ni Klopp tu mwenye uzoefu na fainali. Ni Jurgen Klopp pekee ambaye ana uzoefu na fainali za Champions League, lakini katika fainali 5 za mwisho za Klopp katika michuano yote alipoteza zote, ukiacha Klopp hakuna mchezaji yeyote ndani ya Liverpool ambaye amewahi kucheza fainali za michuano hii.

Ukubwa wa kikosi, Gareth Bale, Asensio na Isco ni aina ya wachezaji ambao mara kadhaa unawaoana katika benchi la Real Madrid, lakini benchi la Liverpool kuna wachezaji wa kawaida sana mfano benchi la Liverpool vs Roma Simon Mignolet, Nathaniel Clyne, Ragnar Klavan, Alberto Moreno, Danny Ings, Dominic Solanke, Ben Woodburn. Aina za mabenchi haya mawili zinaokuonesha namna ukubwa wa timu hizi ulivyo tofauti.

CHANYA.

Arnold Alexender vs Marcelo. Pamoja na kuwawaza kina Mo Salha, Sadio Mane na Roberto Firminho lakini Arnold anaweza kuibeba Liverpool. Katika mechi za usoni ambazo Madrid waliruhusu bao yalipitia upande wa kulia aliko Marcelo. Uwezo wa Alexender Arnold unaweza kuwapa Liverpool faida ya mipira kutoka upande wao wa kulia itakayowasaidia Salah na Firminho kumaliza kazi, mchoro hapo chini unaonesha namna Bayern Munich walivyowafunga Real Madrid.

Tottenham wanawapa imani. Liverpool wanaweza kupata imani kuwafunga Madrid wakikumbuka kwamba Tottenham waliwafunga Madrid katika msimu huu wa Champions League. Tot waliwafunga Madrid kwa counters ambazo ndio aina ya Liverpool wanayowamalizia wapinzani wao wengi msimu huu na hii inaweza kuwapa nguvu zaidi.

Liverpool hawahitaji dakika zote 90. Real Madrid wanaonekana kuchukua muda dakika za mwanzo kusoma mchezo wa wapinzani katika mechi kubwa. Lakini kwa Liverpool wameonekana kumaliza mechi nyingi katika dakika za mwanzo, mchezo vs Maribor walifunga mabao 4(dakika 36 za mwanzo), wakafunga 3 dakika 28 za mwanzo vs Sevilla, wakafunga 3 dakika 19 za mwanzo vs Spartak Moscow, bao 2  katika nne vs Porto, bao 3 katika dakika 19 vs City, na 3 ndani ya dakika 20 vs As Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here