Home Kitaifa Anachotarajia Shaffih Dauda baada ya mabadiliko Simba

Anachotarajia Shaffih Dauda baada ya mabadiliko Simba

9751
0
SHARE

Jumapili Mei 20, 2018 klabu ya Simba imefanya mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya mabailiko ya katiba yao ili kuendana na mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Wanachama wa Simba kwa pamoja wamepiga kura ya ndio kupitisha mabadiliko ya katiba yao ili kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu ambapo kuanzia sasa klabu hiyo itaendeshwa kwa mfumo wa hisa.

Mwekezaji Mohammed Dewji amechukua hisa asilimia 49 na wanachama wengine wamebaki na hisa 51%.

Baada ya mabadiliko hayo ya mfumo na katiba ndani ya Simba, Shaffih Dauda amesema tatizo la vilabu vya Simba na Yanga sio mfumo tatizo ni watekelezaji wa mfumo husika.

“Tatizo la Simba na Yanga siamini kama ilikuwa ni mfumo uliokuwepo, mfumo si tatizo wanaoingia kwenye mfumo kwa ajili ya utekelezaji ni akina nani?

“Mfumo unaweza ukabadilishwa lakini inapokuja suala la utekelezaji hapo ndio kwenye tatizo. Ukifuatilia vizuri sio tatizo kwenye mpira peke yake, ‘human capital’ ni tatizo kubwa la nchi.”

“Tunachotarajia kuona ni Simba mpya yenye vitega uchumi, viwanja, hostels, academies, uongozi unaoeleweka, ili hayo yote yawezekane wanahitajika watu wenye taaluma na uwezo wa kutekeleza hivyo vitu.”

“Hongera kwa wanasimba kwa kukubali kufanya mabadiliko ya mfumo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here