Home Kitaifa Simba, Mo wamalizana kibingwa

Simba, Mo wamalizana kibingwa

11563
0
SHARE

Leo Jumapili Mei 20, 2018 klabu ya Simba imefanya mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya mabailiko ya katiba yao ili kuendana na mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Wanachama wa Simba kwa pamoja wamepiga kura ya ndio kupitisha mabadiliko ya katiba yao ili kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu ambapo kuanzia sasa klabu hiyo itaendeshwa kwa mfumo wa hisa.

Mwekezaji Mohamed Dewji amechukua hisa asilimia 49 na wanachama wengine wamebaki na hisa 51%.

Mkutano huo wa mabadiliko ya katiba ya Simba ulihidhuriwa na Waziri mwenye dhamana ya michezo Dr. Harrison Mwakyembe  ambaye alikuwa mgeni rasmi, vilevile alikuwepo Mkurugezi wa michezo Yusuph Singo kutoka Wizara ya michezo, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura huku TFF ikiwakilishwa na mkurugenzi wa ufundi Salum Madadi.

Kaimu Rais wa Simba Salum Abdallah ambaye pia alitoa hotuba fupi kabla ya hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mwakyembe.

Dr. Mwakyembe amesema amepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wa Simba wakipinga kuchakachuliwa kwa katiba yao ya mwaka 2016.

Tumepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama, wanachama wanadai kuwa, katika katiba yenu ya mwaka 2016 baadhi ya mambo yameingizw kinyemela ambayo hayakujadiliwa katika mkutano mkuu halisia.”

Sisi tulidhani katika mkutano wa leo hayo ya nyuma wala yasingekuwa na msingi sana lakini wametupa siku saba msajili asipoifuta hiyo katiba basi watatuburuza mahakamani.”

Mimi naomba nitoe ushauri wa bure kwa wanasimba hawa wachache sana, hasa katika kipindi hiki cha kutetea ubingwa wa Simba. Mtu au mwanachama unapokwazwa na jambo fulani jitahidi sana kutumia njia za utatuzi zilizo kwenye katiba yenu wenyewe.”

Mkifiata hili Simba hakuna mtu atakaewafuata duniani, lakini ukiona katiba yenu imekunyima uhuru na haki kwa maoni yako tumia sheria ya BMT na kanuni zake. Kabla haujakimbilia mahakamani ile sheria inasema ukiwa na matatizo, mamlaka ya juu ya rufani ni Waziri mwenye zamana ambaye ni mimi hapa.”

Bahati mbaya hawa ndugu zangu hawakuniletea mimi wanatishia kwenda mahakani, suala lenyewe ukiliangalia ni rahisi sana. Nawahakikishia kama mpo hapa hilo tatizo lenu hata dakika tano siwezi kuchukua ntakuwa nimelimaliza.”

Wasijitokeze hapa kuanza kuleta maneno yao, pitisheni katiba yenu hapa leo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here