Home Kitaifa Sababu JPM kupewa jezi namba 19

Sababu JPM kupewa jezi namba 19

8487
0
SHARE

Klabu ya Simba imetoa zawadi ya jezi mbili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa lengo la kumshuru kukubali kuwakabidhi kombe la ligi kuu msimu huu 2017/18.

Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah amemkabidhi ezi mbili Waziri mwenye dhamana ha michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ili afikishe zawadi hiyo kwa Rais.

Jezi moja imeandikwa namba 19 na jina la Rais’JPM’ lakini jezi nyingine imesainiwa na wachezaji wote wa Simba pamoja nanviongozi.

Kaimu Rais wa Simba ameeleza kwa nini wamempa Rais jezi yenye namba 19 mgongoni na si namba nyingine.

“Lengo la zawadi ni kuonesha kwamba tumetoa shukrani kwa kukubali kuja kushiriki nasi, hilo ni jambo la kwanza.”

“Namba 19 ina maanisha kwamba huu ni ubingwa wetu wa 19 wa ligi kuu kwa hiyo ni kumbukumbu kwake kwamba yeye alitukabidhi ubingwa wa kombe la ligi la 19 nchini.”

Bw. Abdallah amesema jezi iliyosainiwa na wachezaji na viongozi wote ni zawadi nzuri na itadumu kwa muda mrefu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here