Home Kimataifa #RoadToRussia, Brazil wako vizuri lakini hili linaweza kuwamaliza Urusi

#RoadToRussia, Brazil wako vizuri lakini hili linaweza kuwamaliza Urusi

10136
0
SHARE

Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kinachokwenda Urusi kinaonekana kama kikosi ambacho kinaenda kuwasha moto. Uwepo wa vijana wengi wenye vipaji vikubwa sana inawapa matumaini Wabrazil kubeba ndoo.

Lakini Dani Alves hayupo, na Alves ni pengo tena pengo haswa. Sahau kuhusu uongozi wake anapokuwa uwanjani na experience aliyonayo katika mashindano mbali mbali lakini Brazil watamiss mengi zaidi.

Tangu kocha Tite aipewe Brazil mwaka 2016 katika mechi 19 alizoisimamia, Alves alikosa michezo 5 tu na kati ya mechi 3/5 ambazo Alves alizikosa zilikuwa za kirafiki na hii inakuonesha namna ambavyo Alves alikuwa muhimu.

Ukitoa mechi hizo 5 kunabaki 14 ambazo Alves aliichezea Brazil wakati Tite akiwa kocha, katika mechi hizo 14 ni mchezo mmoja tu ambao Alves hakucheza dakika 90 na tena mchezo huo alikosa dakika 7 tu, ilikuwa vs Russia.

Katika michuano mingi ambayo Wabrazil walibeba kombe la dunia, walinzi wa Brazil wamekuwa sehemu muhimu sana kwao na wamekuwa chanzo kikubwa kwa mafanikio ya Brazil.

Roberto Carlos na Cafu hawa wawili hadi hivi sasa ukienda miji kama Rio Di Jeneiro pale Brazil wanawapa heshima kubwa sana Malegend hawa na wanaamini ndio walikuwa chachu kubwa kwao kuwa mabingwa 1970 na 2002.

Mwaka 1994 goli la mkongwe wa zamani wa Brazil Romario lilitokana na uwezo mkubwa wa mlinzi wa Brazil Jorginhos Beckham-esque katika nusu fainali, 2010 hapo alikuwepo Maicon moja ya walinzi ambao walifanya vizuri sana.

Kwa taarifa tu ni kwamba tangu mwaka 1986 wakati wa kombe la dunia nchini Mexico, Brazil hawajawahi kwenda kombe la dunia na beki ambaye hakutarajiwa kama ambavyo wanakwenda Urusi.

Uwezo wa walinzi haswa wa kulia wa Brazil unanifanya kutoshangaa pia uwepo wa Maril Fernandez katika kikosi cha waandaaji wa michuano ya kombe la dunia Urusi, Fernandez ni kati ya wachezaji muhimu wa Urusi lakini ana uraia wa Brazil.

Baada ya yote haya Tite ameamua kuweka karata yake kwa Fagner, na hawa wawili Tite na Fagner wanajuana tangu wakiwa Corithians, wengi wanataraji Danilo kuanza katika timu ya Brazil mechi chache katika Epl zinaweza kumfanya kukaa benchi na akimuangalia Fagner akianza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here