Home Kitaifa Nduda baada ya rekodi ya Simba kuvunjwa mikononi mwake

Nduda baada ya rekodi ya Simba kuvunjwa mikononi mwake

9704
0
SHARE

Goli pekee la Edward Christopher kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar limehitimisha rekodi ya Simba kucheza mechi za ligi msimu huu bila kupoteza mcjezo.

Golikipa wa Simba Said Mohamed ‘Nduda’ alianza kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa ligi kuu na kujikuta rekodi ya Simba ya kutopoteza mchezo ijiharibika mikononi mwake amesema haimuulizi kichwa sana kwa sababu ni matokeo ya mchezo wa soka.

Siwezi kusema kwamba najisikia vibaya kwa sababu mambo haya ni sehemu ya matokeo ya mchezo, Kagera Sugar walikuwa na lengo la kushinda na sisi pia tulikuwa na lengo la kushinda mwisho wa siku yanabaki kuwa matokeo ya mpira.

“Kwa upande wangu nimeona ni jambo la kawaida kimchezo.”

Aishi Manula alikosekana katika mchezo huko kwa sababu ya kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here