Home Ligi EPL Shaffih Dauda anaamini Mikel Arteta anafaa kuwa mrithi wa Wenger

Shaffih Dauda anaamini Mikel Arteta anafaa kuwa mrithi wa Wenger

12039
0
SHARE

Taarifa ambazo zinazidi kuenea kuhusu kocha atakaevaaa viatu vya Arsene Wenger kuifundisha Arsenal zinamhusisha mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Mikel Arteta ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa Manchester City chini ya Pep Guardiola.

Tetesi nyingi kutoka vyombo vya habari vya Ulaya zinasema Arteta anapewa nafasi kubwa ya kumrithi babu Wenger mara tu atakapoondoka Emirates.

Shaffih Dauda anaamini Arteta ni mtu sahihi ambaye ataisaidia Arsenal kutoka ilipo sasa kwa sababu ni mtu anaefahamu vitu vingi kuhusiana na klabu hiyo ikiwa ni pamoja na falsafa ya timu.

“Watu wengi walikuwa wanataka Arsenal impate kocha mwenye kariba ya Arsene Wenger lakini wanasahau kwamba, Wenger wakati anakwenda Arsenal hakuwa na jina kubwa sana kama alivyokuja kulipata baada ya kuwa Arsenal.”

“Wenger alikuwa anafundisha Japan, namna alivyoingia Arsenal haikuwa imepangwa lakini kuna-coincidence ilitokea wakati Wenger amekwenda London kwa ajili ya likizo akakutana na David Dein wakati ule wakapiga story wakawa washkaji.”

“Huo ushkaji ndio uliopelekea hata wakati Bruce  Rioch anatoka moja kwa moja David Dein akaamua kumvuta Wenger, yaliyofuatia sote tunayajua.”

“Kwa hiyo nakukumbusha hata Arteta wakati anakwenda Arsenal kama mchezaji, watu wengi hawakuamini kama alikuwa mtu sahihi wa kuziba nafasi ya viungo ambao walikuwa wameondoka. Fabregas alikuwa amekwenda Barclelona, Samir Nasri ambaye alikuwa amekwenda City na Abou Diaby ambaye alikuwa anaumiaumia sana.”

“Lakini miaka miwili tu Arteta alikuwa tayari amejiimarisha kwenye timu akapewa na kitambaa cha unahodha jambo ambalo halikuwa dogo. Akawa-prove wrong wale ambao walidhani angeshindwa kuvaa viatu vya wale mabwana. Wakati huo ilikuwa imepita miaka mingi bila Arsenal kuchukua taji lakini katika kipindi chake Arsenal walichukua FA Cup mara mbili.”

“Naona hata sasa hivi wanampa timu kwa style ileile, watu wanasahau kwamba mfumo wa timu hauwezi kubadilika mara moja. Hawezi kuja mtu mpya akaianzisha Arsenal mpya huyu ni aina ya watu ambao falsafa zao zinaendana kabisa na misingi ya Arsenal ambayo tayari imeshawekwa.”

“Mashabiki wote wa Arsenal ukiwauliza kwa nini wanaipenda timu yao watakwambia ni timu inayocheza mpira wa kuvutia wa pasi nyingi na kushambulia kwa style yao ya kupendeza kwa hiyo hakuna namna atakuja mtu wa kuja kuibadili hiyo.”

“Kwa Arteta ametoka La masia amekaa na Pep Guardiona na amekuwa nahodha chini ya Arsene Wenger, hata Guardiola si kwamba alitoka timu kubwa, lakini leo hii mkubwa. Zidane anaandika historia, wakati anapewa Real Madrid tulikuwa tunamzungumza hivihivi kutoka timu B anapewa timu kubwa lakini kinachoendelea sasa hivi ni historia.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here