Home World Cup Tiketi ya Bombadia: Neymar na Pogba wataanzia viwanja hivi

Tiketi ya Bombadia: Neymar na Pogba wataanzia viwanja hivi

9895
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

*Inaendelea….* WAKATI ambapo makocha wa timu za taifa wakiendelea kutaja vikosi vyao, vile rasmi na ambavyo si rasmi kwaajili ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia. Tayari watu wa Soka wamepata mkanganyiko baada ya kikosi cha Ufaransa, kilichoitwa na Didier Deschamps.

Haya ndio mambo yaletayo muhamko katika fainali hizi, tukianzia tu hapa kwenye chaguzi za vikosi. Tuachane na Ufaransa, ngoja tuendelee na makala yetu ya Viwanja 12 ambavyo vitatumika katika Kombe la Dunia.

Tunaendelea na kiwanja cha saba, baada ya Nizhny Novgorod tulicho kizungumzia siku ya jana.

*Rostov Arena*

Rostov Arena ni moja ya Uwanja ambao unapatikana katika mji wa Rostov-On-Don. Uwanja huu ni mpya na umefunguliwa hivi karibuni kwaajili ya fainali hizi za Kombe la Dunia.

Mipango ya ujenzi huu ilitoka baada ya nchi ya Urusi kupata nafasi ya kuwa wenyeji wa kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018. Na mji wa Rostov-On-Don ukachuguliwa kwamba moja ya viwanja ambavyo vitatumika katika fainali hizi, utajengwa hapo.

Mpango wa mwisho wa kupatikana kwa Mhandisi wa Uwanja huo ulifanyika mwaka 2012 na mwaka 2013 kazi za ujenzi zilianza.

Rostov Arena ulikamilika rasmi mwaka 2017, lakini Uwanja huo ukafunguliwa mwaka 2018 tarehe 15 Aprili katika mchezo wa Ligi kuu kati ya Rostov dhidi ya Khabarovsk.

Uwanja huu una idadi ya kuingiza watu 45,000 hii ni maalumu kwa fainali za Kombe la Dunia, lakini baada ya kumalizika kwa fainali hizi Uwanja huu utapunguzwa mpaka kufikia idadi ya kuingiza watu 25,000.

Baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia Uwanja Rostov Arena utamilikiwa na klabu ya FC Rostov kwa matumizi ya mechi za nyimbani. Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi tano tu katika fainali hizi zitakazoanza mwezi ujao:

★17 June 2018 21:00 – Brazil vs Switzerland – Group E

★20 June 2018 18:00 – Uruguay vs Saudi Arabia – Group A

★23 June 2018 21:00 – Korea Republic vs Mexico – Group F

★26 June 2018 21:00 – Iceland vs Croatia – Group D

★2 July 2018 21:00 – 1G vs 2H – Round of 16

Hizi ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika Uwanja wa Rostov Arena, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here