Home Kitaifa Shaffih Dauda baada ya JPM kukubali kwenda uwanjani “kuna kitu nakiona kwa...

Shaffih Dauda baada ya JPM kukubali kwenda uwanjani “kuna kitu nakiona kwa mbali”

10172
0
SHARE

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba na Kagera Sugar utatumika kuwakabidhi Simba kombe la ubingwa wa VPL ambapo mgeni rasmi katika mchezo huo atakuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pome Magufuli.

Kuelekea mchezo huo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kutoa hamasa kwa Rais Magufuli.

“Kesho Mh. Rais atakuwa mgeni rasmi katika uwanja wetu wa taifa kushuhudia mechi ya Simba na Kagera Sugar katika kilele na kukabidhiwa kombe kwa hiyo nimeona ni jambo kubwa ambalo halijawahi kutokea nikiwa mkuu wa mkoa lakini pia katika serikali yetu ya awamu ya tano kumpata Rais anashiriki michezo ni jambo kubwa sana.”

“Nawaalika wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na nje ya Dar kushiriki kwa kikamilifu katika mechi ya kesho kati ya Simba na ndugu zetu wa Kagera lakini pia kushuhudia Simba wakipokea kombe na wakikabidhiwa na Rais.”

“Naamini siku ya kesho inaweza kuwa ni ya mapinduzi kwa upande wa michezo hususan mchezo wa mpira wa guu kwa sababu mkubwa akiwepo hata mambo yetu yale ya changamoto za michezo tulizonazo itakuwa ni nafasi kwa viongozi wa michezo watakaokuwepo kumnong’oneza mzee kwamba tuangalie na huku.”

Kwa upande wake Shaffih Dauda, kitendo cha Mh. Rais kwenda uwanjani anakiona kama fursa kwa wadau wa michezo na huenda ikawa ni mwanzo wa mambo mzuri kwa serikali kutoa ushirikiano wa juu upande wa michezo.

Timu zetu mara nyingi zimekuwa zinakosa support ya moja kwa moja kutoka serikalini lakini unapoona fursa kama hii ya Rais kwenda uwanjani kuna kitu ambacho unakiona kwa mbali.

Mh. Rais ameona mapungufu yaliyopo, kuna wakati niliwahi kusema kwamba, hatutakiwi kuilaumu serikali kwa kutokushiriki kwenye mambo ya michezo. Sisi wadau wa michezo hatujatengeneza mazingira ya kuishawishi serikali isogee, mambo yetu yanafanyika hovyohovyo na ujanjaujanja mwingi.

Juzi tumemsikia Karia akizungumzia TFF kufanya kazi kwa uwazi na utawala bora na namna ambavyo amedhamiria kutoa makandokando ambayo yamezoeleka. Inawezekana imemshawishi Rais ameamua kwenda uwanjani kuonesha support.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here