Home Ligi EPL Manchester United inavyopiga mkwanja na kutuachia somo VPL

Manchester United inavyopiga mkwanja na kutuachia somo VPL

10947
0
SHARE

Hivi karibuni umetoka mgawanyo wa mapato mbalimbali kwenye ligi kuu ya England, katika mgao huo pesa nyingi zimetokana na haki za matangazo ya television.

Mgao umezingatia vipengele tofautitofauti na hapa ndio kwenye utamu wenyewe. Ligi imemalizika, kuna bingwa na timu zinazoshuka daraja kwa kuangalia mgao namna ulivyo licha ya Manchester City kuwa bingwa wa EPL lakini ipo nyuma ya Manchester United katika mgao wa fedha.

Manchester United inaongoza katika mgao wa fedha, hii ni kutokana na mechi nyingi za Man United muoneshwa kwenye TV kuliko timu nyingine yoyote. Mechi 28 za Man United zilioneshwa kwenye TV wakati Man City mechi zake 26 ndio zulioneshwa kwenye TV.

Mechi nyingi za Man United kuoneshwa kwenye TV kuliko za City, hii ni moja sababu inayoleta utofauti kwenye mgao wa mapato ya haki za matangazo televizion.

Kwa faida ya msomaji kwa sababu hata sisi ligi yetu inaonekana kwenye TV, tunaweza kujifunza jambo. Kwa nini Manchester United pamoja na kushika nafasi ya pili kwenye ligi lakini kwenye mgao anachukua mzigo mrefu zaidi kuliko bingwa?

Wenzetu wamegawa zile pesa katika makundi manne, zile pesa zikiwa kwenye ‘kapu’ kila timu inapata mgao sawa ambapo kila timu inapata paundi milioni 34,812,555 kutokana na haki za matangazo ya television kwa mechi zinazoonekana ndani ya visiwa vya Uingereza.

Kuna mgao unatoka kwa TV zinazoonesha nje ya Uingereza kwa mfano Fox TV, SPN, DSTV na nyingine huku napo kuna kiasi cha pesa kinacholingana ambacho timu zinata  amcho ni kiasi cha paundi milioni 40,771,108.

Sehemu ambayo inaleta utofauti ndio inatuonesha kwa nini ligi yao inakuwa na ushindani. Pamoja na hayo yote wakaweka vipengele halafu wakasema kila mechi ambayo iyaongezeka kwa mfano mechi 10 zimeonekana kwa kila mechi inayoongezeka baada ya 10 kila mechi ina thamani hake hapo ndipo tofauti inapokuja na utaona kwa nini Man United imevuta mkwanja mrefu kuliko Man Cith kwa sababu kila mechi inayozidi inaweka kibindoni kiasi cha paundi milioni 1,129,879.

Kwa hiyo mechi mbili zilizoongezeka una zidisha mara mbili, halafu sehemu nyingine ambayo inaleta utofauti wa gawio ni kwenye msimamo wa ligi, kila nafasi ina mzigo wake tofauti.

Sisi tunajifunza nini? Timu ambayo mechi zake zote zinaoneshwa kwenye TV inapata mgao sawa na timu ambayo mechi zake zinazooneshwa kwenye TV hazizidi 15.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here