Home Kitaifa Kocha mpya Yanga asaini mkataba na kuondoka

Kocha mpya Yanga asaini mkataba na kuondoka

11418
0
SHARE

Kocha Zahera Mwinyi baada ya kuwasili kwa lengo la kuifundisha klabu ya Yanga ilionekana alikuwa bado hajasaini mkataba, hatimaye kocha huyo amesaini mkataba wa kuifundisha  klabu hiyo.

Hussein Nyika mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga amethibisha kocha huyo kusaini mkataba wa miaka miwili.

“Tumemalizana na mwalimu siku ya Ijumaa amesaini mkataba kwa ajili ya kuifundisha Yanga lakini kesho (Jumamosi) anataraji kuondoka kwenda DR Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa kwa sababu mwalimu huyo tulimchukua wakati yupo kwenye majukumu ya kitaifa.”

“Kwa hiyo anakwenda kutimiza majukumu yake kwa sababu timu ya DR Congo ina mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Nigeria weekend ijayo.”

“Atarejea Tanzania baada ya wiki moja kutoka kwenye mechi ya kirafiki kati ya DR Congo dhidi ya Nigeria.”

Nyika amefafanua kwa nini Zahera alikuwa haikai kwenye benchi la ufundi la Yanga katila mechi zilizochezwa tangu alipowasili Yanga.

“Nafikiri watu walikuwa hawaelewi kwa sababu gani mwalimu alikuwa anashindwa kukaa kwenye benchi, ni kwa sababu hakuwa na mkataba, huwezi kupata kibali cha kufanya kazi kama hauna mkataba wa kufanya kazi sehemu ambayo unatakiwa kufanya kazi.”

“Baada ya kusaini mkataba, kuanzia Jumatatu tunashughulikia vibali vyake kwa ajili ya kuitumikia Yanga. Kwa hiyo mpaka atakapo rudi atavikuta vibali vitakuwa tayari na ataanza kukaa kwenye benchi la Yanga.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here