Home VPL Youthe Rostand anawaza mashamba yake

Youthe Rostand anawaza mashamba yake

9231
0
SHARE

Azizi-Mtambo 15

Youthe huku kwetu kuna kitu kinaitwa mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Urefu wako ndiyo kamba yako. Lakini fahamu ukijivuta sana kamba itakatika utaliwa na fisi. Youthe sisi tunaokaa Viti vya VIP kuna washkaji hawapigi makelele kabisa. Wao wanaongea taratibu sana nadhani huwasikiagi. Lakini maneno wanayoongea juu ya kiwango chako ni makubwa. kuna mmoja alisema sijui kubwa nini sitaki kumalizia maana najua kiwango chako. tuachane na hayo Youthe.

Youth Rostand, amekuwa goli kipa ambaye wakati anasajiliwa na klabu ya Yanga, akitokea African Lyon msimu wa mwaka 2016/17, chini ya kocha Mzambia George Lwandima. Alisaini mkataba wa miaka 2 kuitumikia klabu hiyo ndo kwanza ana msimu mmoja na klabu hiyo. Wakati anasajiliwa wengi waliamini kuwa goli kipa huyu ataisaidia klabu hiyo katika michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo. Hivi karibuni walikuwa wanafanya vibaya lakini amekuwa akifanya makosa makubwa mno akiwa golini. Anasifa kubwa ya kuwa goli kipa kutokana na umbo lake kubwa, urefu wake, lakini amekuwa ndo sehemu kubwa ya matatizo.

Youthe Kamtok brother.. Hebu Njoo tuongee.. Youthe Kule Cameroon kuna makabila 250 lakini tumekuona wewe tu huoni ajabu?

Nimemshuhudia baadhi ya mechi za ligi kuu Tanzania bara, Kw mfano mchezo dhidi ya Singida United, Mbeya city, amekuwa mvivu mno kucheza mipira ya kona, Mpira ya adhabu ndogo. Labda pengine anawaza hana mpinzani katika klabu ya Yanga, ambaye ataweza kumpa changamoto. Sawa lakini anadhani Ramadhani kabwila ni kipofu haoni madhaifu ya kaka yake? Kabwili ni kipa mzuri anayechezea timu ya taifa chini ya umri wa miaka 20. Anahitaji uzoefu wa hali ya juu kutoka kwa Yanga bado anahitaji muda.

Kabwili anatumiwa kama kipa wa akiba klabuni hapo kuna baadhi ya michezo ameanza kutokana na Rostand, kupata majeraha. Michezo kama dhidi ya Welayta Dicha, uliofanyika Taifa jijini Dar es salaam.

Turudi kwa Rostand, katika michezo ya kimataifa tuanze na ule wa kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers Fc, uliofanyika uwanja wa Taifa. Mchezo huo uliishia kwa mabao 2-1 Yanga kufungwa, kutokana na uzembe wa goli kipa huyo. Amekuwa akifanya makosa ambayo yana wagharimu Yanga, pale inapokutana na washambuliaji wajanja wenye ustadi mkubwa wa kufunga mabao.

Turudi kwenye mchezo wa kombe La shirikisho barani afrika, Yanga dhidi ya Sport Rayon, mchezo huo ulikuwa wa kundi D. Mchezo huo umeisha kwa sare ya 0-0 Rostand, alifanya makosa ya ajabu sana kama iwashambuliaji wa Sport Rayon basi Yanga wangetulia, angefungwa bao 2 na kuendelea. Yanga inahitaji iingie sokoni na kumleta kipa mwengine ataweza kuleta changamoto zaidi eneo la goli kipa.

Mwalimu mpya wa klabu ya Yanga, Zahera Mwinyi, nilimsikia akisema Rostand, golikipa mzuri ila anahitaji apunguze makosa lakini mimi nasema umri wake ni kwenda kusimamia mashamba yake tu.

Youthe amezaliwa Bafoussam ambao ni mji wa tatu kwa ukubwa kule Camerooni. Mji huo una watu asili yao hapo zamani walitokea Misri wajulikanao kama Bamileke. Katika mji huu wengi wao ni wakulima wa kahawa na mahindi. Rostand ana miaka 32 unadhan hataki kwenda kuangalia mashamba yake?

kaka Youthe sijakusamilia wakati naandika, …How Na… najua kwenu mnasimiana huku mtu anabusu hewani. Nikutakie kila la kheri safari yako ya Bafoussam ila kabla hujafika hebu ondoka na mbegu za mahindi huku kwetu ukajaribu kwenu. Jaribu katumani inastawi sana. Au tukupe na kahawa ka kigoma na ya Rombo ukajaribu kule.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here