Home Kimataifa RvP aitaja mechi ngumu kabisa kuwahi kucheza maishani

RvP aitaja mechi ngumu kabisa kuwahi kucheza maishani

10406
0
SHARE

Moja kati ya washambuliaji hatari kuwahi kutokea katika ligi ya Epl ni Robin Van Persie, Van Persie maarufu kama RvP alikuwa nyota chini ya Arsene Wenger na baadae akawika tena chini Louis Van Gaal akiwa Manchester United.

Kwa sasa Robin Van Persie anacheza katika timu ya kwao ya Uholanzi katika klabu ya Feyenoord bado ana kumbukumbu kubwa kuhusu ligi ya Uingereza, Van Persie anaamini mechi ngumu zaidi kwenye maisha yake aliicheza EPL.

Ni Stoke City, Van Persie anaamini tangu aanze soka katika ngazi ya uweledi hajawahi kucheza mchezo mgumu au kwenda safari ngumu kama safari ya kwenda Britannia Stadium kuikabili Stoke City.

Van Persie ameuelezea mchezo wao dhidi ya Stoke City kwamba ilikuwa kama vita kwa namna Stoke walivyokuwa wanacheza, na takwimu zinaonesha kweli RVP alikuwa na kipindi kigumu Britannia kwani katika mechi 6 katika dimba hilo alipoteza 3,suluhu 2 na kushinda1 tu.

Swansea, Bolton na Sheffield United ni timu nyingine ambazo Van Persie hatakuja kuzisahau, na kubwa anasema ni namna ambavyo timu hizo hazitoi nafasi kwa washambuliaji wa timu pinzani kuwa huru na kila ulipo wanakuwa wanakufuata na kucheza rafu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here