Home Kimataifa #RoadToRussia,Kikosi cha Uingereza chaiingiza Manchester United kwenye rekodi 

#RoadToRussia,Kikosi cha Uingereza chaiingiza Manchester United kwenye rekodi 

8699
0
SHARE

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate ametangaza kikosi cha timu ya taifa Uingereza, katika kikosi hicho Joe Hart pamoja na Jack Wilshaire  wakitoswa katika kikosi hiko caha Three Lions.

Phil Jones, Ashley Young, Jesse Lingard, ma Marcus Rashford  ni wachezaji kutoka klabu ya Manchester United ambao wametangazwa katika jeshi la Southgate linaloelekea Urusi kwenye michuano hii ya kombe la dunia.

Uwepo wa wachezaji wa Manchester United katika kikosi cha Southgate unaifanya Manchester United kuwa klabu ya kwanza kutoa wachezaji kwa ajili ya michuano mikubwa kwa Uingereza mfululizo kuanzia 1950.

Klabu za Liverpool na Tottenham zinaifuatia Manchester United lakini zote mbili zilikosa mashindano mawili mawili, Tot walikosa kuitwa timu ya taifa mwaka 2014, Liverpool walikosa 1986 na wote wawili walikosa 1954.

Japokuwa United wana rekodi hiyo lakini katika kikosi cha Uingereza safari hii klabu ya Tottenham ndio inaongoza kuwa na wachezaji wengi zaidi katika timu ya taiga ya Uingereza(wachezaji 5).

Na Liverpool bado wanashikilia rekodi ya kupeleka wachezaji wengi zaidi katika timu ya taifa ya Uingereza katika michuano mikubwa, hii ilikuwa mwaka 2014 ambapo Liva walipeleka wachezaji 6 katika timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya Euro.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here