Home World Cup Road 2 Russia: Kiwanja utakachomuona Messi hiki hapa

Road 2 Russia: Kiwanja utakachomuona Messi hiki hapa

7155
0
SHARE

⚽TIKETI YA BOMBADIA⚽

*Safari Ya Urusi*

Na: DANIEL S.FUTE

*Inaendelea….* BADO tunasonga na muendelezo wa makala hii ya Viwanja 12, ambavyo vitachezewa mechi za fainali za Kombe la Dunia msimu huu wa 2018.

Tunaendelea na kiwanja cha sita, baada ya Kazan Arena tulicho kizungumzia siku ya jana.

*Nizhny Novgorod*

Nizhny Novgorod ni moja ya Uwanja ambao unapatikana katika mji wa Nizhny Novgorod, huu ni Uwanja mpya katika mji huo uliochukua miaka mitatu kwa kujengwa.

Uwanja huu umejengwa maalumu na Serikali ya mji huo, na pendekezo kubwa la Uwanja huu lilitolewa na Gavana wa mji huo Valery Shantsev. Ambaye baada ya kutoa mamlaka ya kujengwa kwa Uwanja huo akasema nje ya mchezo wa Soka lakini Uwanja huu utatumika katika mashindano mengine ya michezo.

Ujenzi rasmi wa Uwanja huu ulianza mwaka 2015 na kukamilika miaka mitatu baadaye, yaani mwaka 2018. Uwanja wa Nizhny Novgorod ulikuwa sehemu ya jitihada za Kirusi kukaribisha fainali za Kombe la Dunia ya mwaka 2018.

Halmashauri iliufungua rasmi Uwanja wa Nizhny Novgorod tarehe 15 Aprili 2018, katika mchezo wa Ligi kuu kati ya Fc Olimpiyets na Zenit II.

Baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia, Uwanja wa Nizhny Novgorod utatumika rasmi kwa mechi za nyumbani za klabu ya Fc Olimpiyets inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Soka Urusi.

Uwanja huu una idadi ya kuingiza watu 45,000 katika mashindano yeyote ya kimichezo. Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi sita tu katika fainali hizi zitakazoanza mwezi ujao:

★18 June 2018 15:00 – Sweden vs Korea Republic – Group F

★21 June 2018 21:00 – Argentina vs Croatia – Group D

★24 June 2018 15:00 – England vs Panama – Group G

★27 June 2018 21:00 – Switzerland vs Costa Rica – Group E

★1 July 2018 21:00 – 1D vs 2C – Round of 16

★6 July 2018 17:00 – W49 vs W50 – Quarter Final.

Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika Uwanja wa Nizhny Novgorod, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here