Home Kitaifa Karia ametangaza utaratibu mpya TFF

Karia ametangaza utaratibu mpya TFF

10501
0
SHARE

Rais wa TFF Wallace Karia amesema chini ya utawala wake TFF itakuwa ikifanya kazi kwa uwazi ikiwa ni pamoja na kuweka bayana mapato ya shirikisho hilo kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

Karia amesema TFF inafanya kazi kwa karibu na serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo Tanzania.

“Fifa na Caf kila tunapokuwa kwenye vikao wanasisitiza ushirikiano wa mashirikisho yetu na serikali, kwa hiyo tunatambua mdau mkubwa ni serikali ndiyo maana hata mashindano ya Caf U17 hatukupewa kuwa waandaji bila kupata idhini ya serikali”- Wallace Karia, Rais wa TFF.

“Ndiyo maana toka nimeingia mimi nafanya kazi kwa karibu sana na Baraza la Michezo, Waziri mwenye dhamana ya michezo na tumemwalika Rais kuonesha kwamba tuko pamoja na serikali na tutasimamia masuala yote ambayo Rais anasimamia ya kuondoa ufisadi ili kila senti inahokuwepo TFF inatumika kwa maslahi ya mpira na sio maslahi binafsi.”

“Hatuwaogopeshi isipokuwa ndio hali halisi ilivyo sasa hivi, tunacheza ngoma ambayo Tanzania inaicheza sasa hivi.”

“Taarifa zetu za kwanza za hesabu zetu za TFG tutazipeleka kwa msajili kama ambavyo inastahili lakini pia hata kwenye tovuti yetu tutaiweka, tunapeleka Fifa ambapo wataiweka kwenye tovuti yao pamoja na Caf.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here