Home Kitaifa Ufafanuzi wa TFF usajili wa Salamba Yanga

Ufafanuzi wa TFF usajili wa Salamba Yanga

11809
0
SHARE

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amefafanua namna Yanga wanavyoweza kufanikisha kumsajili na kumtumia mshambuliaji wa Lipuli Adam Salamba kwa mujibu wa kanuni.

“Ukisoma kanuni za ligi yetu ya Vodacom kuna kipengele kinairuhusu TFF kutoa leseni wakati wowote kwa kuzingatia maslahi ya timu inayowakilisha kwenyemashindano ya kimataifa.”

“Yote hayo lazima yafanyike kwa  mujibu wa makubaliano kati ya timu aliyokuwa anacheza mchezaji dhidi ya timu anayokwenda kuichezea ambayo inashiriki mashindano ya kimataifa lakini kuwe kuna mazingira maalum ya kuweza kufanikisha jambo hilo.”

“Kwa hiyo kanuni zetu za ligi kuu zipo wazi kwa jambo hilo, tumepata copy kutoka Yanga kwamba wanamuomba Salamba lakini hawajatuambia kama wameshakubaliana na Salamba ili TFF tujue hatua ambazo tunaweza kuwasaidia Yanga kulingana na kanuni za Caf ili waweze kuwatumia hao wachezaji ambao wanawahitaji.”

Salamba alikuwa anacheza Stand United akasajiliwa na Lipuli kadika dirisha dogo la usajili kwa hiyo endapo atajiunga na Yanga atakuwa anacheza timu ya tatu ndani ya msimu mmoja. Kidao amefafanua pia kuhusu jambo hilo na kusema wataishauri Yanga nini cha kufanya.

“Tutakapokuwa tayari tutawashauri Yanga ni nini ambacho wanaweza kufanya ili waweze kutimiza azma yao pamoja kwamba kanuni zetu za ligi kuna kipengele kinatoa mazingira maalum kuweza kutoa leseni kwa mchezaji ili aweze kuwakilisha klabu ambayo inacheza mashindano ya kimataifa na tuliweka kwa makusudi maalum.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here