Home World Cup Road 2 Russia: Fahamu kiwanja watakachocheza Pogba, Iniesta na Ozil

Road 2 Russia: Fahamu kiwanja watakachocheza Pogba, Iniesta na Ozil

9230
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

*Inaendelea….* Tukiwa bado tunaendelea na muendelezo wa makala hii kuhusu viwanja 12, ambavyo vitachezewa fainali za Kombe la Dunia. Sio vyema ni kiacha kukumbusha kwamba, zimesalia siku 28 tu kuanza kwa fainali hizi huko nchini Urusi.

Leo tunasonga mbele kutazama kiwanja cha tano, ambacho kitachezewa fainali hizi.

*Kazan Arena*

Kazan Arena ni moja ya Uwanja ambao upo katika mji wa Kazan, katika Jamhuri ya Tatarstan. Uwanja huu unasimamiwa na klabu ya Rubin Kazan, ambayo inashiriki katika Ligi kuu ya Urusi.

Uwanja wa Kazan ulianza kujengwa mwaka 2010, na ulipofikia mwaka 2013 ulikamilika na ukafunguliwa rasmi.

Uwanja wa Kazan Arena upo Kaskazini-Mashariki mwa jiji la Kazan, kwenye ukanda wa Mto Kazanka ambapo ni kilomita 6 kutoka katikati mwa Kazan.

Kazan Arena ulifunguliwa rasmi katika ufunguzi wa sherehe za 27 za Summer Universiade. Lakini baada ya Uwanja huo kufunguliwa haukuweza kutumika katika mchezo wa mpira miguu hadi kufikia Mei 26 2014 katika mchezo wa kirafiki wa Urusi na Slovakia.

Mwaka 2015, Uwanja huo ulikuwa na michuano ya FINA World Aquatics, ambapo ikalazimika Uwanja huo Soka kuwekewa mabwawa mawili ya kuogelea kwaajili ya michuano hiyo ambayo ilikuwa ikiendelea katika Uwanja wa Kazan Arena.

Kazan Arena una uwezo wa kuingiza watu 45,000 na ndicho kiwango bora cha FIFA, katika mashindano makubwa ya Soka. Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi sita tu katika fainali hizi zitakazoanza mwezi ujao:

★16 June 2018 13:00 – France vs Australia – Group C

★20 June 2018 21:00 – Iran vs Spain – Group B

★24 June 2018 21:00 – Poland vs Colombia – Group H

★27 June 2018 17:00 – Korea Republic vs Germany – Group F

★30 June 2018 17:00 – 1C vs 2D – Round of 16

★6 July 2018 21:00 – W53 vs W54 – Quarter Final

Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika Uwanja wa Kazan Arena, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here