Home Kitaifa Rais Magufuli amekubali kuwakabidhi kombe Simba

Rais Magufuli amekubali kuwakabidhi kombe Simba

10750
0
SHARE

Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magifuli amekubali kuwa mgeni rasmi siku ya Jumamosi katika mchezo wa ligi kuu kati ya Simba na Kagera Sugar.

Mchezo huo utatumika kuwakabidhi Simba kombe la ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2017/18 ambapo Dtk. Magufuli anatarajiwa kukabidhi kombe hilo kwa mabingwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema pia watatumia fursa hiyo kumkabidhi Rais kombe la ubingwa wa CECAFA waliotwaa vijana wa Serengeti Boys nchini Burundi.

“Kwa TFF ni tukio kubwa kwa Rais kutukubalia ombi letu, tunamshukuru sana Waziri mwenye dhamana kwa juhudi kubwa alizozifanya hadi Mh. Rais kukubali ombi letu kwa sababu tunajua anamajukumu mengi ya kitaifa lakini kwakuwa ni mwanamichezo kaona si vibaya kujumuika na watanzania kwa lile tulilomuomba.”

“Tunaamini vijana wetu itakuwa ni zawadi kubwa kwao kukabidhi kombe na kupeana mikono na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kitu kikubwa sana kwa vijana wetu hivyo tunaamini itakuwa motisha kwa ajili ya mashindano yaliyo mbele yao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here