Home Kimataifa Baada ya mechi 403, hatimaye Atletico Madrid wampa kombe Torres

Baada ya mechi 403, hatimaye Atletico Madrid wampa kombe Torres

8974
0
SHARE

Takwimu zinaonesha mji wa Madrid ndio mji unaoongoza kwa makombe mengi ya ligi ya Ulaya katika miaka hii 10, mji wa Madrid kumeenda makombe ya Ulaya 6 katika wakati huu na hii ni baada ya Atletico Madrid kubeba Europa usiku wa leo.

Alikuwa Antoine Griezman dakika ya 21 kuanza kuifungia Atletico Madrid, hili likiwa bao lake la 7 katika michuano ya Ulaya kwa Atletico na kumfanya kuhusika katika mabao 11 ya Atletico katila michuano ya Ulaya(mabao 7 na assist 5).

Dakika ya 49 Griezman aliifungia bao linginie Atletico na kumfanya kuivunja rekodi yake ya ufungaji kwa Atletico ya mabao 7 aliyofunga msimu uliopita michuano ya Ulaya na sasa anakuwa aemfunga mabao 8 msimu huu.

Dakika 1 kabla ya mchezo kuisha Gabi aliipatia Atletico bao la 3, na kuifanya Atletico kuwa mabingwa wapya mbele ya Marseille ambao walikuwa katika ardhi yao ya nyumbani nchini Ufaransa.

Hii ilikuwa clean sheet ya 200/397 kwa Diego Simeone ndani ya Atletico Madrid lakini pia ikiwa clean sheet ya 92/109 kwa mlinda mlango Jan Oblak. Hii ni kama zawadi kwa mchezaji mkongwe Fernando Torres ambaye katika michezo 403 aliyoitumikia Atletico Madrid hili lilikuwa kombe lake kubwa la 1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here