Home Kimataifa You Tube kuonesha fainali ya Champions League buree

You Tube kuonesha fainali ya Champions League buree

7978
0
SHARE

Bado siku chache tu ambapo macho na masikio ya kila mpenda soka duniani yataelekezwa mjini Kiev, Liverpool watakuwa wakicheza dhidi ya Real Madrid katika mchezo huu kumpata bingwa wa Champions League msimu huu.

Sasa shirika la michezo la BT Sports limeamua kuuonesha mchezo huu bure kabisa, kupitia channel yao ya You Tube BT Sports wataonesha mechi hii moja kwa moja kutoka mjini Kiev na ni data tu ndizo utatumia.

Katika fainali ya msimu uliopita ya Champions League kati ya Real Madrid vs Juventus BT Sports walivutia jumla ya watazamaji 6.5m dunia nzima na wanaamini safari hii uwepo wa klabu toka Uingereza utaongeza watazamaji.

Katika kutanua wigo wa kuongeza watazamaji, mchezo huu pia utaoneshwa katika application ya BT Sports pamoja na website yao, na yeyote mwenye app hiyo ataweza kuuona mchezo huo moja kwa moja kutoka Kiev.

Peter Oliver ambaye ni mkurugenzi wa BT Sports amekiri kwamba uwepo wa Liverpool katika fainali hii ni fursa kubwa katika biashara ya uoneshaji mpira na wataitumia fursa hiyo kuongeza mashabiki dunia nzima.

Tarehe 26 mwezi huu ndio siku ambayo wababe hawa wawili watatoana jasho, timu zote mbili zimeshindwa kuchukua ubingwa katika ligi zao za ndani na hii inaweza kuwa nafasi yao kuweka heshima.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here