Home Brazuka Kitaani TP Mazembe yaendelea kumtesa Msuva

TP Mazembe yaendelea kumtesa Msuva

12715
0
SHARE

Timu anayocheza kijana wa kitanzania Simon Msuva imepoteza mechi yake ya kombe la vilabu bingwa Afrika baada ya kufungwa 2-0 na TP Mazembe ukiwa ni mhhezo wa pili wa Kundi B.

Msuva alikuwa anakutana kwa mara ya tatu dhidi ya Mazembe akiwa na vilabu viwili tofauti na mara zote timu anayoitumikia imeshindwa kupata mayokeo. Alicheza dhidi ya TP Mazembe mara mbili akiwa mchezaji wa Yanga katika kombe la shirikisho Afrika.

Juni 28, 2016 Msuva akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga alikuwepo wakati timu yake inapoteza  mechi kwa kukubali kufungwa 1-0 kwenye uwanja wa taifa.

Mechi ya pili Msuva akiwa Yanga walipoteza kwa kichapo cha 3-1 wakiwa ugenini Agosti 23, 2018 DR Congo.

Wakati Difaa El Jadida inapoteza mechi kwa kufungwa 2-0 kwenye uwanja wake wa nhumbani, Simon Msuva alikuwepo kwenye kikosi cha Difaa, yeye alikuwa anapoteza mechi yake ya tatu dhidi ya Mazembe.

Baada ya Difaa kufungwa 2-0 na TP Mazembe sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Kundi B ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here