Home World Cup Road 2 Russia: Una taarifa kuhusu viwanja vya kombe la dunia?

Road 2 Russia: Una taarifa kuhusu viwanja vya kombe la dunia?

11295
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

*Inaendelea…* HUU ni mwendelezo wa makala yetu, ambapo tunazungumzia Viwanja 12 ambavyo vitachezewa katika fainali za Kombe la Dunia mapema mwezi ujao huko Urusi.

Kwa kawaida Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’, wao wapo makini kuchagua viwanja ambavyo vitatumika katika mashindano makubwa ya mchezo wa mpira wa miguu, ni lazima vifikie viwango vya kuanza kuingiza watu 35,000 na kuendelea.

Tayari tumepata elimu ya kutosha katika viwanja vitatu nyuma ambavyo tayari nimesha vielezea. Leo tunaendelea na kiwanja cha nne ambacho nacho ni chaguo la ‘FIFA’ katika fainali hizi za Kombe la Dunia.

*Ekaterinburg Arena*

Ekaterinburg Arena ni moja ya Uwanja ambao upo katika mji wa Yekaterinburg, mkoa wa Sverdlovsk Oblast.
Mji huu unakadiria kufiki idadi ya watu 1,349,772 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010. Ni moja ya miji ambao yenye watu wengi sana katika nchi ya Urusi.

Uwanja huu ulijengwa maalumu kwa michezo yote kwa ujumla, ambayo ilikuwa ni sahihi kufanyika katika eneo la uwanja huo. Ulijengwa mwaka 1957 na moja ya michezo ambayo ilikuwa ikifanyika katika Uwanja huu wa Ekaterinburg, ni mchezo wa mbio za baiskeli,Soka na Mpira wa Tenesi.

Baadae Uwanja huu ukamilikishwa rasmi na klabu ya Ural Yekaterinburg, ambayo ni klabu inayotoka katika mji huo huo. Uwanja huu ulianza kuingiza idadi ya watu 35,696 lakini baada ya kuchaguliwa na ‘FIFA’ kwaajili ya matumizi ya fainali za Kombe la Dunia ukaongezwa mpaka kufikia idadi ya watu 45,000.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi nne tu katika fainali hizi ambazo zinatarajia kuanza Juni 14, mechi hizo ni:

★15 June 2018 17:00 – Egypt vs Uruguay – Group A

★21 June 2018 17:00 – France vs Peru – Group C

★24 June 2018 20:00 –
Japan vs Senegal – Group H

★27 June 2018 19:00 – Mexico vs Sweden – Group F

Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika Uwanja wa Ekaterinburg Arena, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.

~ *Official_DSK*

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here