Home World Cup Road 2 Russia: De gea akiri kuwa mpira haufai

Road 2 Russia: De gea akiri kuwa mpira haufai

15294
0
SHARE

Hii ni orodha kwa ufupi ya aina ya mipira iliyowahi kutumika Kombe la dunia.

1930 – Tiento & T- Model
Kule nchini Uruguay wakati fainali za kombe la dunia za kwanza kabisa zikipamba moto kwanza hakukua na mpira maalumu hadi pale karika mchezo wa fainali. katika Mchezo wa Fainali kati ya Uruguay na Argentine, Mapema mpira uliokuwa ukichezeka ulijulikana kama Tiento ambao uliletwa na Waargentine.

Tiento

wakati mpira wa waArgentine ukiwa uwanjani walikuwa wanaongoza Mabao mawili 1. Baadae mpira ukabadilishwa ukaletwa huo wa T-model ambao ulitengenezwa na wauruguay, Argentina akafa tatu kwa mbili.

T-model

1934 – Federdale 102
Kombe la pili liliandaliwa kule nchini Italia. kipindi hiki Bwa Benito Musolini aliagiza serikali yake kitengenza mipira ya Federdale 102. hata hivyo baadhi ya mipira kutoka Uingereza wa aina hiyo hiyo pia ilitumika.

Mpira huu ni ule ule wa Uruguay ulibadilishwa kwa kuwekwa leya nzuri ya pamba ambayo ilitoa fursa kwa wachezaji kupiga mipira ya vichwa bila wasiwasi wowote tofauti na ule wa awali.

1938 – Allen
kwa mara ya kwanza kampuni binafsi ya kifaransa ilipewa nafasi ya kuandaa mipira kwa ajili ya kombe la dunia. Mpira huu ulikuwa na muonekano kama ule wa awali ambapo kwa mbali unafanana na mpira wa kikapu. mpira wa mwanzo ulishonwa kwa vipande 12 lakini huu wa Allen ulishonwa kwa vipande 13.

Baadae mpira huu ulionekana kubadilishwa tena hadi kufika vipande 18 ili kujaribu kukidhi mahitaji ya wachezaji.

1950 – Duplo T
ilipita zaidi ya miaka 12 ndipo kombe la dunia kurudi tena baada ya Vita vya dunia kuchukua nafasi kubwa. Mpira huu ulitumika hapo awali kwenye ligi za Nchini Argentine kabla haujabadilishwa jina na kuitwa Superval. Baadae kampuni hiyo iliondoka nchini huko na kwenda Brazil ambapo mpira ulibadilishwa tena jina na kuotwa Superball.

Katika kipindi cha miaka 12 kila kampuni ilijitahidi kuandaa mpira ambao utaonekana bora na kupata tenda ya kusambaza mipira hiyo. Wajuvi wa mambo wanadai katika historia ya soka mpira uliokuwa mlaini na wa kisasa kwa nyakati zile ambapo unaweza kufananishwa na mipira ya sasa ni hii ya Duplo T. ulikuwa mlaini na haukuwa na mikwaruzo kama ule wa awali.

1954 – Swiss Wolrd Champion
kombe la Dunia lilipopelekwa Uswisi basi kampuni ya Kost Sport ilipata ujiko wa kuandaa mpira bora kabisa. Mpira huu ulikuja na mbwembwe mbalimbali ikiwemo zig zag kwenye vipande vyake.

ulikuwa wa njano na ulikuwa na vipande 18. tatizo kubwa ni kwamba FIFA ilikata kampuni yoyote kuweka jina lake kwenye mipira ile.

1958 – Top Star
Kombe hili lilichezwa Swedeni.FIFA iliendelea kushikilia sera yake ya kukataza makampuni kuweka majina yao kwenye mipira. wakati huu FIFA ilitangaza ofa kwa makampuni kutuma sampo za mipira yao pamoja na bahasha ya jina la kampuni. Makampuni 102 yalipeleka sampo zao. Kamati ya FIFA ikishirikiana na taifa la Sweden walifanya upembuzi na makampuni yalibaki 10 tu.

Mpira namab 55 ndio uliotangazwa kuwa mshindi. Kila mshiriki wa kombe la dunia alipewa mipira 30. Brazil walinunua mipira mingi zaidi. Kampuni hiyo ilijulikana kama Angelholm. Mpira wa Top Star ndio mpira pekee uliotumika kwenye makombe ya dunia mawili.

1962 – Crack
ukiachana na Jabulani mpira uliolalamikiwa zaidi mpira mwingine uliopigwa sana vita ni huu. Ulitumika kombe la dunia kule Chile. ulijengwa kwa Vipande 24 ambavyo vilikuwa na mduara tofauti na ya awali.

Kampuni ya Custudio Zamora ya chile ndio waliotengenza mpira huu. Nchi za ulaya ziliupiga vita mno. Top Star ulipendwa zaidi na kutumika badala ya Crack.

1966 – Challenge 4-Star
kombe la dunia wakati ule lilifanyika England. Mipira 111 ilitolewa kushindanishwa kisha Challenge ukashinda. ulikuwa na vipande 25.

1970 – Telstar
hili lilikuwa kombe la kwanza la dunia kurushwa dunia nzima. Sasa kama una babu yako aliwahi kukwambia alionekana kombe la dunia kabla ya hapo basi huyo babu fix. Hii ilikuwa kwa mara ya kwanza kampuni ya Addidas ilipata tenda ya kutengeneza mipira ya kombe la dunia kule Mexico.

Mpira wa kwanza kabisa ambayo muundo wake unatumika hadi leo ndio huu ulikuwa wa kwanza. ulikuwa na rangi nyeupe na nyeusi na ulikuwa na vipande tofauti kabisa na mipira ya hapo awali.

1974 – Telstar Durlast
Kampuni ile ile ya Addidas ilipewa tenda. iliboresha zaidi mpira huu ambao uling’aa zaidi kisha iliwekwa leya nzuri ambayo itahimili unyevu nyevu na joto kali.

hata hivyo baada ya hapo Addidas kwa Mara nyingine walipewa nafasi ya kutumia jina lake kwenye mipira hiyo.

1978 – Tango
Mpira wa hapo awali ulionekana kuzidiwa zaidi na Mvua.

wakati huu Addidas walijitahiddi na kuweka leya nyingine tofauti ili kupambana na maji.

Mipira mingine ni.

1982 – Tongo Espana

1986 – Azteca
1990 – Etrusco Unico
1994 – Questra
1998 – Tricolore
2002 – Fevernova
2006 – Teamgeist

2010 – Jabulani
ni mpira ambao ulisemekana kuwa unapotezwa sana na upepo licha ya baadhi ya wachezaji kuutumia vyema. Mpira huu ulifanyiwa uchunguzi hadi na shirika la Mambo ya anga la Marekani ambapo walidai kuwa ulikuwa na kasi sana hewan. Fifa walidai kuwa jabulani ndio mpira uliokuwa na mduara sahihi zaidi kwani ulikuwa na vipande 8.

Casilas alisema ule mpira una kisirani haukai mkononi. Cesar alisema ulikuwa kama kigololi mkononi. Hata hivyo FIFA walidai kuwa mpira ule ulifanyiwa majaribio kwa muda wa miezi sita chini ya Ballack na Lampard.

2014 – Brazuca

2018 – Telstar 18
huu ndio utakaotumika mwaka huu. Reina na De gea wamesema haufai ni mgumu kudaka..

imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here