Home Kimataifa MJADALA: Salamba anakidhi vigezo kucheza Yanga?

MJADALA: Salamba anakidhi vigezo kucheza Yanga?

13788
0
SHARE

Yanga imeiandikia barua Lipuli ikiomba kumtumia mshabuliaji Adam Salamba katika masindano ya kinataifa (Caf Confederation Cup) ambapo Yanga ipo hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kanuni za Caf zinairuhusu Yanga kuongeza mchezaji/wachezaji endapo haijatimiza idadi ya wachezaji 30, mjadala uliopokwa sasa ni je, kanuni zinamruhusu Salamba kuitumikia Yanga?

Kupitia kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM, kulikuwa na mjadala kuhusiana na Salamba kama anasifa au hana sifa za kucheza Yanga kipindi hiki ambacho madirisha yote ya usajili Tanzania yalishafungwa.

Mlamu Ng’ambi ambaye amewahi kuhudumu Simba katika nafasi tofauti ikiwemo kamati ya usajili, amefafanua jambo hilo kwa utaalam na uzoefu wake wakati akihojiwa na Sports Xtra.

“Kwa mujibu wa taratibu za Caf, mchezaji yeyote unayeweza kumtumia kwenye mashindano ya Caf lazima awe na licence ya local league. Adam salamba ana leseni ya Lipuli, dirisha la usajili limeshafungwa kwa hiyo kuna ugumu kwa Yanga kuweza kumtumia kulingana na taratibu ambazo Caf wanazitumia.”

“Nakumbuka kipindi wakati nipo Simba kwenye kamati ya usajili hili jambo tulilizungumza sana,  klabu yoyote ambayo itakuwa haijatimiza wachezaji ambao wanatakiwa (30) kwa mujibu wa taratibubzetu, iruhusiwe kufanya usajili hata katikati ya ligi.”

“Madirisha ya usajili Afrika yapo tofauti-tofauti kutokana na nchi kwa hiyo ikitokea klabu inapoteza mchezaji katikati ya ligi halafu kwa mfano dirisha la usajili Tanzania limefungwa mwezi wa nane au tisa halafu timu iliuza mchezaji maana yake haitaweza kusajili mchezaji mwingine hadi litakapofunguliwandirisha dogo mwezi wa 11 au 12.”

“Lakini timu ingeruhusiwa kusajili kwa sababu haijatimiza idadi ya wachezaji maana yake kungekuwa na hiyo nafasi kwakua kanuni zetu zilikuwa zinaturuhusu kufanya hivyo lakini kanuni zetu zimetubana kwamba mchezaji lazima awe na leseni ya ligi ya ndani na kipindi cha usajili kimeshafungwa.”

Shaffih Dauda akaja na hoja kwamba, kama Caf wenyewe wameruhusu inawezekana ma-TMS managers wanaweza mufungua mifumo ya usajili na kuidhinisha mchezaji akaingia kwenye mfumo kwa sababu jambo hili ni maalum ambalo Caf wenyewe wameruhusu.

“Mimi ni TMS Manager wa zamani wakati mfumo huo ndio unaanzishwa labda taratibu kama zimebadilishwa.”

Kuna jambo jingine ambalo limeibuka kwamba, mchezaji mmoja hawezi kucheza zaidi ya vilabu vitatu ndani ya msimu mmoja. Salamba alikuwa anacheza Stand United akasajiliwa na Lipuli kipindi cha usajili wa dirisha dogo, anapotoka Lipuli kwenda Yanga itakuwa ni timu ya tatu.

Ng’ambi amesema hata kanuni za Caf zinambana, itabidi Salamba apewe leseni ya Yanga ambayo ndio itakuwa klabu yake ya sasa ili awe na sifa ya kucheza.

Alex Luambano akakumbushia kwamba kuna kipindi Monja Liseki na Alphonce Modest walienda kucheza Yanga katika mazingira kama haya ambayo Salamba anatakiwa na Yanga.

“Wakati huo hakukuwa na kanuni kama za sasa,  kwa utaratibu ambao naufahamu, kuna baadhi ya nchi zina ruhusu kama hujatimiza idadi ya wachezaji 30 unaruhusiwa kuongeza hata kanuni za Caf zinasema hivyo lakini mchezaji huyo lazima awe na leseni ya ligi ya ndani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here