Home Kimataifa Kumbe Supu ya Chura ndiyo ilikuwa ikimfanya Park Ji Sung kuwa na...

Kumbe Supu ya Chura ndiyo ilikuwa ikimfanya Park Ji Sung kuwa na nguvu uwanjani

9368
0
SHARE

Zamani nilikuwa nikisikia hadithi za kuhusu Wakorea, Wachina au Wajapan kula vitu kama vyura na nyoka sikuwa nikiamini. Lakini sasa kwa hadithi hii ya Park Ji Sung inanifanya kuogopa hata kwenda China nisije kula nyoka.

Wengi tunamkumbuka Park Ji Sung, alikuwa kati ya viungo ambao walionekana kuwa na nguvu sana uwanjani. Park alikuwa akihaha uwanja mzima kutafuta mpira na alikuwa akionekana kuwa fiti na kutochoka mda wote.

Park ambaye kwa sasa yuko nchini kwao Korea ya Kusini baada ya kustaafu kucheza soka mwaka 2014, ametoboa siri moja ambayo inaweza ikashangaza umati wa watu lakini kwake anaona poa tu.

Park anasema wakati akiwa mdogo hakuwa na nguvu sana na wala hakuwa imara sana, baba yake alisikia kwamba vyura wanasaidia kuongeza nguvu, na mchuzi wake unamfanya mtu kuwa imara zaidi.

Ilimbidi baba yake kuanza kuzunguka sehemu mbali mbali za vijijini ili kutafuta vyura hao ambao walikuwa wakisemekana kusaidia kuongeza, na alipowapata alitengeneza mchuzi maalum kwa ajili ya mwanae.

Ji Sung anasema ladha ya mchuzi huo ilikuwa ni mbaya sana, lakini kwa kuwa alitaka kuwa mwanasoka mkubwa siku za mbeleni ilimbidi tu kunywa mchuzi huo na anaamini ulisaidia sana kumuimarisha.

Park Ji Sung alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Asia kuwahi kushinda michuano ya Champions League chini ya Sir Alex Ferguson na pia akashinda ubingwa wa EPL mara 3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here