Home Kitaifa Kinachofuata baada ya Simba kupata mwekezaji

Kinachofuata baada ya Simba kupata mwekezaji

12007
0
SHARE

Kuna watu wanaweza kuwa wanajiuliza maswali, tangu Simba imeridhia kuingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu na kumpata mwekezaji umepita muda bila kujua nini kinaendelea baada ya hayo yote.

Uongozi wa klabu hiyo umetangaza mkutano wa wanachama Mei 20, 2018, kabla ya siku hiyo Mlam Ng’ambi mmoja wa viongozi ambao walihusika kuzunguka sehemu mbalimbali kutoa elimu ya mfumo mpya wa hisa ameeleza nini kinafuata baada ya kupata mwekezaji.

Ng’ambi wakati anazungumza na Sports Xtra ya Clouds FM amesema kinachofuata sasa ni utekelezaji wa kutengeneza mfumo ili uweze kufanya kazi.

“Hapo nyuma tulikuwa tunatoa elimu kwa ajili ya wanachama wetu waweze kuelewa mfumo haswa ambao utakuja kuingia na mwekezaji wetu ambaye amepatikana.”

“Sasa tunakwenda kwenye utekelezaji wa kutengeneza ule mfumo ili uweze kufanya kazi, ili ufike huko lazima twende kwenye mkutano maalum kwa ajili ya kubadilisha baadhi ya vipengele kwenye katiba yetu ili viweze kuturuhusu kutengeneza huo mfumo ambao utaanza kufanya kazi baada ya katiba kuwa imepiishwa.”

“Ni mchakato mrefu kidogo ambao unahusisha mambo mengi ya kisheria na kitaalam ndio maana kwa kipindi fulani imeonekana ni jambo ambalo lipo kimya lakini kuna kazi kubwa sana ilikuwa inafanyika ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa sababu kutengeneza mfumo ni jambo ambalo linahitaji uangalifu wa hali ya juu.”

“Tunakwenda kwenye mkutano Mei 20 kwa ajili ya kuipitia katiba yetu na kuibadilisha ili ituruhusu kwenda kwenye mfumo kamili.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here