Home Kimataifa Changamoto 4 za Tuchel ndani ya PSG

Changamoto 4 za Tuchel ndani ya PSG

10719
0
SHARE

Tayari klabu ya PSG imemtangaza Thomas Tuchel kama kocha wao mpya, Tuchel anachukua mikoba ya Unai Emery ambaye pamoja na kuipa ubingwa wa Ligue 1 PSG lakini hatakuwa nao msimu ujao, Tuchel ana changamoto nyingi PSG lakini hizi 5 ni lazima azitibu haraka.

1.Neymar. Panga upangavyo matatizo ya PSG lakini hili lazima likae namba moja, Neymar ni mungu mtu PSG na lazima alelewe kwa namna ambayo hata mabosi wa timu watafurahia lakini pia kocha wa timu lazima amfanye Neymar kuwa chini yake. Kuna tishio kwamba anakwenda Real Madrid/Man United na Tuchel anatakiwa kumfanya Neymar apapende PSG.

2.Wachezaji hasara kwa timu. Kuna wachezaji PSG wanalipwa pesa nyingi sana tofauti na wanachokifanya katika klabu, Pastore, Layvin Kurzawa, Thiago Silva na Angel Di Maria wamekuwa na kiwango duni siku za usoni lakini wanalipwa pesa nyingi sana, hili ni suala ambalo pia Tuchel anatakiwa kulimaliza na hii inaweza kuwaweka nyota hawa njia panda katika kikosi hicho.

3.Plan B. Unai Emery alikosa Plan B katika kikosi cha PSG, kila mchezo alikuwa akiitumia 4-3-3 kama mfumo mama wa PSG. Katika mechi kubwa haswa za Champions League PSG walionekana wa kawaida dhidi ya makocha wengine wakubwa na Unai alikosa mbinu mbadala kuifanya PSG ipambane na timu kubwa, Tuchel ni kati ya tactic masters katika soka la sasa na anahitajika kutafuta mbinu nyingine kuichezesha PSG.

4.Chipukizi. Klabu kama PSG sera yao ya usajili inawaweka mashakani kuhusu adhabu ya kufungiwa kusajili. Unai alijaribu kwa wakina Rabiot na Alphonse Areola lakini nyota wengi kutoka academy ya PSG walipotezewa. Tuchel anahitaji kutafuta damu changa kuibeba PSG katika hali kama hizi, kwa sasa mchezaji mtoto wa raisi wa Liberia George Weah aitwaeTimothy Weah pamoja na Yacine Adli wanaonekana wanatakiwa kuanza kuwa lulu chini ya Tuchel.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here