Home Dauda TV Video-Ubingwa wa Simba biashara

Video-Ubingwa wa Simba biashara

10928
0
SHARE

Jamani kuna watu wanajua kucheza na fursa, ubingwa wa Simba VPL 2017/18 kuna watu wanafanya biashara wanaingiza ‘mtonyo’ na maisha yanaendelea kama kawaida.

Jumamosi Mei 12, 2018 kulikuwa na game ya ligi kui kati ya Singida United dhidi ya Simba pale Namfua Stadium, Singida. Katika pitapita za hapa na pale Dauda TV ikakutana na matukio kadhaa ambayo yalikuwa yanaendelea nje ya uwanja huku watu wakitengeneza mkwanja.

Unaambiwa baada ya Simba kuifunga Yanga 1-0 tayari watu wakaanza ku-print T-shirts ‘Simba Bingwa 2017-2018’ wakijua kwamba Mnyama atashinda taji, baada ya Yanga kufungwa 2-0 na Tanzania Prisons moja kwa moja Simba ikatangaza ubingwa jamaa wakaweka mzigo sokoni wakaanza kupiga pesa.

Wapiga picha nao hawakuwa nyuma wenyewe walichungulia fursa ya ubingwa wa Simba kwa jicho lao, waka-print banner kubwa yenye picha ya wachezaji na kuandika ‘Simba Bingwa 2017-2018’ kwa ajili ya kazi yao.

Bonyeza play kuangalia video hapa chini uwasikie jamaa wanavyotengeneza pesa kupitia ubingwa wa Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here