Home Dauda TV Video-Mashabiki wa Simba walivyoigombea jezi ya Lipuli

Video-Mashabiki wa Simba walivyoigombea jezi ya Lipuli

13129
0
SHARE

Shabiki mmoja wa Simba almanusura avuliwe jezi yake ya Lipuli na mashabiki wenzake wa Simba ambao hawakutaka kabisa kuiona jezi ya Lipuli.

Katika timu zote ambazo zimeshacheza mechi mbili na Simba, Lipuli ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo, timu nyingine kama zilitoka sare mchezo mmoja zilipoteza mchezo mwingine.

Katika mchezo uliochezwa uwanja wa Samora-Iringa, Simba ilitokea kwenye tundu la sindano baada ya Lipuli kuongoza kwa muda mrefu kwa goli lililofungwa na Adam Salamba kabla ya Mavugo kusawazisha.

Baadhi ya mashabiki wa Simba huenda wanaichukia Lipuli kwa sababu endapo Simba wangepoteza mchezo huo huenda ingeongeza presha kwao kuelekea mechi ya watani wa jadi iliyochezwa Aprili 29, 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here