Home Uncategorized Unajua Kante anamkubali nani zaidi?

Unajua Kante anamkubali nani zaidi?

13522
0
SHARE

Kocha msaidizi wa N’golo Kante Piere Ville alisema kuwa kante alikutana na wakati mgumu sana kwani timu nyingi zilikuwa hazimtaki kutokana na umbo lake dogo. Alikuwa anafanya mazoezi ya kukaba kila siku na kukimbia uwanjani kwa zaidi ya masaa matatu ili kujiimarisha. Hata wakati mazoezi ya timu yalipoisha lakini bado alikuwa akifanya mazoezi yake binafsi.

Image result for kante life story kid

Rafiki yake mkubwa Francois Lemoine alisema kuwa “sisi tulikuwa na miaka 18 lakini Ngolo alikuwa na miaka 13 tu na aliweza kucheza kwenye timu ya miaka 18 bila wasiwasi tena kwa ufanisi mkubwa

Alikuwa mdogo kuliko wote kwenye timu lakini hakuna aliyefanikiwa kumpiga chenga au kukimbizana nae. Alikuwa amekomaa haswa. Siku moja mwalimu alimwambia zunguka uwanja mara 50 kwa utani cha ajabu alizunguka mara 150 kuanzia siku ile mwalimu hakuwa kumpa maelekezo tena maana waliamini wazi kwamba likuwa a uwezo mkubwa.

Image result for kante life story kid

Mashabiki walijaa uwanjani kumwangalia kama kituko kutokana hasa na umbo lake na kwa namna alivyocheza uwanja mzima. Mwaka 2010 alipata shavu la kucheza Boulogna.

Image result for kante boulogne

Kocha wake akasema Kante alikuwa hapangiwi kitu cha kufanya uwanjani. Alikuwa anacheza uwanja mzima. Ndoto zake za kuchez aligi kuu England hatimae zilitimia. Klabu ya Leicester City ilianza harakati za kusaka huduma yake.

Image result for kante and steve walsh

Steve Walsh aliyetimiza ndoto za Akina Jarmie Vardy na Riyadh Mahrez alianza harakatai za kukamilisha dili la Kante kujiunga na the Fox. Mwezi wa nane mwaka 2015 alikamilisha usajili wake na kujiunga na Leicester kwa ada ya paundi 5.6 milioni.

Kante ametokea familia ya watoto wanne. Yeye ni mtoto wa kwanza kwao. Baba yake alifariki akiwa na miaka 11 kisha akachukua majukumu ya kuilea familia yake akiwa kama baba. Alijua matunda ya kufanya kazi kwa bidi hivyo hakuwahi kujilaumua aiha kwa kuanguka au kukosa. Alijtoa kwa roho yale yote na ngvu zake zote kuhakikisha anapata kidogo kitu kwa ajili ya familia yake.

Magazeti mengi ya ufaransa yalimpachika jina la makelele Claudio kutokana na aina yao ya uchezaji. Makelele alipokuwa Nantes alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake mkubwa na jitihada alizoonesha na kumfanikisha kujenga jina kubwa lililompelekea kucheza vilabu vikubwa duniani.

Lakini Ngolo Kante alipoulizwa kuhusu kufananishwa kwake na makelele alisema hapana. “mimi namkubali sana Lassana Diarra. Nimejifunza mengi kupitia kwake. Ninachokilenga mimi ni kuwa kiongozi na mfano wa kuigwa kwenye timu, sio tu uwezo wa kukaba ila napaswa niwe na mchango nje ya hapo.

Kante hakuwahi kuabudu magari ya kifahari wala nguo za fasheni za bei ghali. Alipojiunga mazoezini Chelsea alikwenda na kijigari cha zamani kijulikanacho kama Mini Cooper. Wakati mwingine alitumia vijibasikeli Fulani vidogo maarufu kama Kick Scooter. Hakubadilisha gari lake hilo moja kama la ngama licha ya kwamba alikuwa akipokea mshahara wa Paundi 120,000 kwa wiki. Kibongo bongo hapa kuna washkaji najua wana Ma Ranger Rover kibao utadhani wanaziuza lakini wana maisha ya kawaida.

Hana mambo mengi kwenye suala la nywele. Kwanza alikuwa akimuungisha msela wake wa Leicester aliyekuwa akimyoa nywele ambaye saluni yake ilikuwa kule kule mjini Leicester. Alikuwa anatembea karibu mile 130 ili tu msela wake yule amnyoe. Kante amekuwa na roho ya kutokusahau mahali alipotokea au washakji zake wa zamani.

imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here