Home World Cup Road 2 Russia: Je unayajua haya?

Road 2 Russia: Je unayajua haya?

8462
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

*Inaendelea….*

TAYARI tumepata kushuhudia baadhi ya ligi kuu zikimalizika jana na viwanja vya klabu kufungwa baada ya kutumika katika msimu mzima wa 2017/18. Vinahitaji mpamziko, si mapumziko tu pia marekebisho madogo madogo kama ya kubadilisha nyasi, wenzetu walioendelea hii ni kawaida yao katika viwanja vyao.

Baada ya kuona ubora wa Uwanja wa Saint Petersburg, leo tunasonga mbele tena kutazama uwanja mwingine wa tatu ambao utatumika katika fainali za Kombe la Dunia.

Tayari tumesha vitazama viwanja vya Luzhniki na Saint Patersburg, vimebaki viwanja tisa tu kwaajili ya kuvifahamu vyema na kutambua mechi ambazo zitachezwa katika fainali hizo.

*Fisht Olympic*

Fisht Olympic ni Uwanja ambao upo katika mji wa Sochi. Mji huu unakadiria kufikia watu 343,334 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010.

Uwanja huu ulijengwa maalumu kwa mashindano maalumu ya Olimpiki, ambapo ulifunguliwa mwaka 2013.

Baada ya kufunguliwa mwaka huo, Uwanja huu ulikuwa una idadi ya kuweza kuingiza watu 41,220. Baada ya FIFA kuchunguza na kuuchagua kuwa nao utakuwa moja ya viwanja shiriki za fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, wakaufunga kwaajili ya marekebisho madogo maalumu kwa fainali hizo.

Mwaka 2017 uwanja wa Fisht Olympic ulifunguliwa rasmi na ukafikia idadi ya kuingiza watu 48,000 kwa pamoja.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi sita tu katika fainali za Kombe la Dunia, mechi hizo ni:

★15 June 2018 21:00 – Portugal vs Spain – Group B

★18 June 2018 18:00 – Belgium vs Panama – Group G

★23 June 2018 18:00 – Germany vs Sweden – Group F

★26 June 2018 17:00 – Australia vs Peru – Group C

★30 June 2018 21:00 – 1A vs 2B – Round of 16

★7 July 2018 21:00 – W51 vs W52 – Quarter Final

Hizi ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo Fisht Olympic, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here