Home Dauda TV Video-Okwi awekewa ulinzi kutoa zawadi ya ubingwa

Video-Okwi awekewa ulinzi kutoa zawadi ya ubingwa

10111
0
SHARE

Kabla ya mechi dhidi ya Singida United Jumamosi Mei 12, 2018 wachezaji na benchi la ufundi la Simba walivaa T-shirts maalum za ubingwa wa VPL 2017/18 wakati wa maandalizi ya mwisho (warm-up) kuelekea mchezo huo kwenye uwanjawa Namfua, Singida.

T-shirts hizo mbele zilikuwa na maandishi yaliyosomeka Simba Bingwa 2017-2018 na nyuma zilikuwa zimeandikwa Asante SportPesa.

Baada ya warm-up wachezaji wote na benchi la ufundi walizivua T-shirts na kuwapa mashabiki kama zawadi ya ubingwa wao.

Mashabiki wengi walikuwa wakiitaka t-shirt ya Emanuel Okwi jambo ambalo lilitaka kuzua vurugu, ikabidi polisi wamuwekee ulinzi nyota huyo kwa kumsindikiza adi alipokwenda kumkabidhi t-shirt hiyo kijana mdogo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here