Home Uncategorized kikosi cha Brazil hiki hapa (selecao)

kikosi cha Brazil hiki hapa (selecao)

16388
0
SHARE

HIKI hapa kikosi cha timu ya taifa Brazil, ambacho kitakwenda kupambana nchini Urusi katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Walinda lango:

Alisson (Roma), Ederson (Man City), Cassio (Corinthians).

baada ya Ederson kufanya vyema na klabu ya Man City ni wazi sasa anahitajika kufanya hivyo na timu yake ya taifa.

Walinzi wa Pembeni:

Marcelo (Real Madrid) Danilo (Man City), Filipe Luis (Atletico Madrid), Fagner (Corinthians).

Dank Alves hatokuwepo nchini Urusi. huenda pia ikawa fainali zake za mwisho ambazo alikuwa na uhakika wa kushiriki. Marcelo watapigana Vikumbo na Felipe Luisi huku Fagner akijaribu kupambana nafasi ya beki wa kulia dhidi ya Danilo ambaye nae ametokea katika kikosi cha dhadhabu cha Man City

Walinzi wa kati:

Marquinhos (PSG), Thiago Silva (PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).

hakuna nafasi kwa David Luisi. Silva atapata ushindani mkubwa kutoka wa Marquinhos na Miranda. Bila Shaka Silva na kija huyu wa Gremio wataanzia benchi. Utakuwa msimu mbaya sana kwa David Luiz ambaye amekuwa na maisha ya kusuasusa kwenye kikosi cha Antonio Conte.

Viungo:

Willian (Chelsea), Fernandinho (Man City), Paulinho (Barcelona), Casemiro (Real Madrid), Philippe Coutinho (Barcelona), Renato Augusto (Beijing Guoan), Fred (Shakhtar).

Bwana mdogo Fred aliyehusishwa san na kutua katika kikosi cha Jose Mourinho hatimaye amepata nafasi kwenye kikosi cha Bossi Titte

hata hivyo kuna ushindani mkubwa sana katika nafasi ya katika ambapo Casamero na Fernandinho.

Coutinho itabidi acheze nafasi ya kiungo mchezeshaji zaidi ili kutoa Nafasi kwa Neymar, Jesus, Willian na Firmino kuwa huru zaidi katika safu ya ushambuliaji.

Coutinho atakumbana na ushindani mkubwa kutoka Paulinho.

Wilian na Douglas Costa wataminyana sana.

Washambuliaji:

Neymar (PSG), Gabriel Jesus (Man City), Roberto Firmino (Liverpool), Douglas Costa (Juventus), Taison (Shakhtar).

Shida kubwa kati ya Firmino na Jesus. Mwalimu titte ameonekana kumuamini zaidi Jesus kuliko Firmino na hii ni kutokana na Coutinho, Jesus na Neymar kuonekana kufanya vyema zaidi timu ya taifa.

Hivyo urafiki na muunganiko wao mkubwa unaonekana kumbagua zaidi Mshambuliaji huyu hatari zaidi wa Liverpool

Wachezaji muhimu waliotemwa

David Luis wa Chelsea

lucas Moura

Hulk

Oscar

Ramirez

Gustavo

Dante

Majeruhi

Dan Alves

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here