Home Kimataifa #RoadToRussia, mabingwa wa kuzuia duniani wanaokwenda Urusi mwezi ujao

#RoadToRussia, mabingwa wa kuzuia duniani wanaokwenda Urusi mwezi ujao

10968
0
SHARE

Wazungu wanasema “Good Striker Win A Game But Strong Defence Win A Tittle” yaani ukiwa na washambuliaji wazuri utashinda mechi ila ukikaba vizuri utashinda kombe, kuelekea kombe la dunia nchini Urusi mapema mwezi ujao wapo mabingwa wa kuzuia/kukaba duniani ambao hawa wanaweza kuwa wagumu kufungika.

Soth America. Huku mechi za kufudhu huwa ni nyingi(18), Brazil kabla ya kocha wao Tite kuwasili walikuwa na rekodi ya kufungwa mabao 8 katika mechi 6, lakini Tite alitilia mkazo namna Wabrazil wanaweza kujipanga kutoka katika eneo lao la Ulinzi.

Baada ya Tite kuwasili Brazil waliruhusu mabao 3 tu katika mechi 12 na kwa ujumla wamefungwa mabao 11 katika safari.yao kuelekea Urusi(mechi 18), Miranda akionekana kuwa nguzo yao muhimu zaidi katika eneo la ukabaji, dakika 1440 alizocheza aliwafanya kufungwa mabao 10 tu.

Ulaya, Kutoka bara la Ulaya timu ya taifa ya Hispania na Uingereza ndio zina rekodi nzuri zaidi ya kukaba, Waingerez/Three Lions wenyewe hadi wanapata nafasi kushiriki michuano ya kombe la dunia, nyavu zao ziliguswa mara 3 tu katika michezo yao 10 waliyocheza, katika dakika 810 za golikipa Joe Hart langoni alifungwa mara 3 tu huku beki wao kisiki John Stones yeye dakika 630 alizocheza Uingereza hawakufungwa.

Hispania. Kama ilivyo kwa Uingereza, Hispania nayo ina rekodi nzuri katika eneo lao la kujilinda, tofauti na Uingereza, Wahispania ni bora katika kujilinda kwa kukaa na mpira na hii inawafanya kuchukua alama nyingi kuliko Uingereza(28 dhidi ya 26), na kufunga mabao mengi kuliko Uingereza(36 kwa 18), De Gea naye amecheza dakika 810 akafungwa mara 3, Ramos akicheza dakika 710 akafungwa mara 3.

Afrika, Morocco eneo lao la ulinzi linatupa matumaini ya kombe la dunia, beki kisiki wa Juventus Medhi Benatia amewafanya Morocco kufungwa bao 1 tu katika mechi 8 kuelekea Urusi katika dakika 621 alizoichezea Morocco na mlinda lango wao Munir naye amefungwa bao 1 tu katika mechi hizo, hii ndio timu yenye kukaba vizuri zaidi Afrika.

CONCACAF, huku ndiko waliko Mexico kwa sasa, na michezo yao 16 waliyocheza kuelekea kombe la dunia wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 8 tu japo kuna bao 4 waliruhusu mechi 3, lakini uwiano wao ni bao 2 kila mechi. Hector Moreno ndio beki kisiki kwani dakika 1125 alizocheza waliruhusu mabao 5 tu.

Asia, japo hawapewi nafasi lakini uwezo wa kocha Carlos Queiroz ni mkubwa sana na kumbuka huyu ametumia muda mrefu na legend wa Man United Sir Alex Ferguson, Queiroz ameishape defence ya Iran katika namna ambayo wanakuwa wagumu sana kufungwa na hiki kilichangia wao kwenda Urusi.

Katika michezo 18 ambayo Urusi ilicheza kuelekea Urusi walifungwa mabao 5 tu, Jalali Hossein ana miaka 36 lakini uzoefu wake unamfanya kuwa mlinzi tegemezi Iran, ameshacheza dakika 794 katika mechi za kufudhu na katika dakika hizo ameruhusu wavu kuguswa mara 1 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here